• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wasikilizaji wa Redio China Kimataifa washuhudia mandhari na utamaduni mkoani Guangxi

    (GMT+08:00) 2009-01-19 15:01:42

    Wasikilizaji 9 wa nchi za nje waliopewa tuzo ya mashindano ya chemsha bongo ya ufahamu wa utalii yaitwayo "vivutio vya Guangxi mwaka 2008", walimaliza matembezi yao kwenye mkoa unaojiendesha wa kabila la Wazhuang wa Guangxi, sehemu ya kusini magharibi ya China. Katika matembezi hayo walieleza ufahamu na mawazo yao kuhusu mandhari nzuri ya asili na utamaduni wa kipekee wa wakazi wa mkoa huo.

    Wasikilizaji waliopewa tuzo ya mashindano hayo waliwasili Nanning, mji mkuu wa mkoa wa Guangxi tarehe 29, mwezi Desemba mwaka uliopita, katika matembezi ya zaidi ya wiki moja, wasikilizaji hao walitembelea sehemu nyingi za Nanning, Baise, Liuzhou na Gulin, na waliondoka Guangxi tarehe 7 mwezi Januari mwaka huu.

    Mkoa unaojiendesha wa kabila la Wazhuang wa Guangxi ni mmoja ya mikoa yenye rasilimali nyingi za utalii nchini China. Huko kuna milima na mito mizuri ya Yangshuo, ambayo inasifiwa na watu kuwa "hakuna milima na mito mizuri zaidi duniani kuliko ile ya Gulin", "Tanping", sehemu ya mtoni yenye maji machache, na yenye mchanga na mawe mengi", pamoja na "Shabai", ambayo ni sehemu yenye milima mingi ya mawe ya chokaa, sehemu hizo ni sehemu zisizoonekana katika sehemu yoyote ya duniani.

    Bi. Liao Guangling, ni msikilizaji kutoka Marekani, kabla ya hapo hakuwahi kutembelea Guangxi na kuona mandhari nzuri za maumbile pamoja na utamaduni wa watu wa kabila dogo la huko, alisema hayo ni mazingira mazuri zaidi kuliko waliyosikia katika radio na yalivyoelezwa katika vitabu. Alisema:

    "Safari hii, nimefika Guangxi, nimeona milima na mito yote ya mkoa huo ni mizuri ajabu, milima midogo ni mingi mithili ya mayoga yaliyochomoka baada ya kunyesha mvua, maji ya mito ni maangavu kabisa hata ninaweza kuona chini yake. Vitu vilivyonivutia zaidi ni ukarimu na uchangamfu wa watu wa kabila la Wazhuang, pamoja na uhodari wao katika kucheza ngoma na kuimba. Kila mahali tulipofika, tuliona wasichana wa kabila hilo waliovalia mavazi ya siku kuu, tena walitukaribisha kwa kuimba nyimbo nzuri za kabila hilo."


    1 2 3
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako