• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wasikilizaji wa Redio China Kimataifa washuhudia mandhari na utamaduni mkoani Guangxi

    (GMT+08:00) 2009-01-19 15:01:42

    Alipofika China safari iliyopita, Bw. Le Gia Phong alikaa mjini tu, lakini safari hiyo alipata nafasi ya kushuhudia mila na utamaduni wa watu wa kabila dogo la huko Guangxi, hususan nyimbo za kabila la Wazhuang zimempa kumbukumbu nyingi.Alisema:

    "Kabla ya kufika China safari hii, nilifahamu kidogo mila na utamaduni wa kabila la Wazhuang wa mkoani Guangxi kutokana na kusoma na kukusanya data za maneno na picha husika. Lakini wakati nilipowasili katika sehemu ya vijiji ya Wazhuang, niliburudishwa na nyimbo za wasichana wa kabila hilo, kusema kweli, nyimbo zao ni nzuri sana, licha ya kusikiliza, nilipata nafasi ya kuuliza maswali na kujibiwa na wasichana wa kabila la Wazhuang kwa kuimba nyimbo. Ingawa sauti na mtindo wa nyimbo tulizoimba ni tofauti kidogo, lakini nilihisi uchangamfu na upole wa wasichana wa kabila hilo."

    Ni tofauti na Bw. Le Gia Phong, msikilizaji wetu Bw. Yogeshwar Tyagi kutoka India, anapenda tufe la hariri lililotarazwa, ambayo ni sanaa ya kazi za mikono ya watu wa kabila la Wazhuang wa mkoa wa Guagnxi. Watu wa kabila hilo wana mazoea ya kutupa tufe la hariri, ambayo ilimfurahisha sana Bw. Yogeshwar Tyagi, tena alinunua tufe la hariri wakati alipoitembelea wilaya ya Jiuzhou, ambayo ni mahali pa asili panapotengenezwa matufe ya hariri. Alilsema:

    "Nimefurahishwa sana na kupata kumbukumbu nyingi kuhusu tufe la hariri, ambacho ni kitu muhimu cha kuonesha mapenzi kati ya wavulana na wasichana wa kabila la Wazhuang, nimevutiwa sana na kitu hicho. Tulifurahi sana kwa kupata nafasi ya kutembelea mahali pa asili panapotengenezwa matufe hayo, kwangu mimi huu ni wakati nisioweza kuusahau. Huko niliona ufundi wa jadi wa utengenezaji wa matufe ya aina hiyo na utamaduni wa kikabila, ambao umehifadhiwa vizuri. Wakati nilipoona kila familia, wazee kwa vijana wote wanashughulika kutengeneza matufe maridadi ya aina mbalimbali, nilivutiwa sana."


    1 2 3
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako