• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wasikilizaji wa Redio China Kimataifa washuhudia mandhari na utamaduni mkoani Guangxi

    (GMT+08:00) 2009-01-19 15:01:42

    Bw. Abobakr Mohamed Ali Aboelmagd kutoka Misri, vilevile alivutiwa sana na mandhari nzuri ya asili ya mkoa wa Guangxi. Hususan sehemu ya mlima wa Gulong, ambapo alifurahishwa mno na kusafiri mtoni kwenye mashua, pamoja na mandhari nzuri zilizoko kwenye kando mbili za mto, na ndani ya mapango ya mawe ya chokaa.Alisema:

    "Nilifurahi mno wakati niliposafiri mtoni kwenye mashua. Tulifika kwenye mabonde ya milima, kuangalia mapango ya mawe ya chokaa yenye maumbo ya ajabu, vilevile tulisafiri kwenye maji maangavu ya chemchemi na kuburudishwa na mandhari nzuri ya maumbile, ambayo ninashindwa kuieleza kwa maneno, ninatarajia kwamba nyote mtapata nafasi ya kuona mandhari nzuri ya Guangxi."

    Mkoa unaojiendesha wa kabila la Wazhuang wa Guangxi unapakana na ardhi ya Vietnam. Hivyo ni rahisi kwa watu wa Vietnam kufanya utalii nchini China. Msikilizaji wetu Bw. Le Gia Phong aliwahi kufika Guangxi kabla ya hapo, anaona utamaduni wa nchi hizi mbili una asili moja. Alisema:

    "Maneno ya wimbo mmoja wa nchini Vietnam yanasema, Vietnam China, milima inapakana mito inaungana, kuwa pamoja kando ya bahari ya Mashariki, urafiki wetu ni kama jua la asubuhi, kuonana asubuhi na usiku, kusikiliza pamoja jogoo akiwika asubuhi. Kwa nionavyo, kuna mambo mengi ya namna moja au yanafanana katika utamaduni wa Vietnam na Guangxi, utamaduni wa nchi mbili unatokana na shughuli za uzalishaji mali za wakazi wa huko."


    1 2 3
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako