• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tamasha la jadi la siku kuu ya Taa kwenye mtaa wa Qianmen mjini Beijing

    (GMT+08:00) 2009-02-09 17:03:41

    Tarehe 9 mwezi Februari ni siku kuu ya Taa ya jadi ya Wachina, ambayo ni siku nyingine ya pilikapilika kubwa katika kipindi cha siku kuu ya Spring. Wachina wanasema ikipita siku kuu ya Taa, basi pilikapilika zote za kusherehekea mwaka mpya zinaisha. Katika siku kuu ya Taa, watu wa familia na marafiki hukutana pamoja na kula Yuanxiao ambayo aina ya chakula kinachotengenezwa kwa unga wa mchele laini na kunata, na kuchemshwa katika maji, kuwasha taa za jadi za China, kufanya mchezo wa vitendawili na tamasha la maonesha ya michezo. Katika siku kuu ya Taa ya mwaka huu, maonesho ya michezo ya jadi yataoneshwa kwenye mtaa wa Qianmen, ambao ni mtaa maarufu zaidi nchini China wenye shughuli nyingi za biashara na historia ya zaidi ya miaka 600.

    Mtaa wa Qianmen ni mtaa wa miaka mingi, ambapo maduka mengi yalijengwa kwenye kando mbili za mtaa huu wenye urefu wa mita 840 hivi. Katika miaka mia kadhaa iliyopita majengo ya mtaa huo yamekuwa yakidumisha mtindo wa jadi wa sehemu ya Beijing, kila mwaka kuna idadi kubwa ya watalii wanaotembelea huko kwa kuvutiwa na utamaduni na mambo ya jadi ya China. Mfanya kazi wa kamati ya usimamizi ya mtaa wa Qianmen, Bw. Li Bo alisema,

    "Mtaa wa Qianmen uko upande wa kusini wa lango kubwa la Zhengyang, na ni karibu sana na majumba ya mfalme wa zamani. Hapo zamani kila mara mfalme alipotoka kutembelea sehemu nyingine, ikiwemo kutoa sadaka katika mahali vilipowekwa vibao vya mizimu ya mababu ya jadi, alikuwa hupita kwenye mtaa huo, hivyo mtaa huu pia unaitwa mtaa wa Tian yaani 'mtaa wa mbinguni', kwani mfalme anaamini yeye ni mtoto wa mbinguni. Mtaa wa Qianmen ulianza kujulikana katika karne ya 16 au 17, na ulistawi polepole baada ya enzi ya Ming, na ulifika kileleni katika enzi ya Qing, tangu ulipojengwa hadi hivi sasa mtaa huu una shughuli nyingi za biashara, na maduka yanaongezeka bila kusita."


    1 2 3
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako