• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tamasha la jadi la siku kuu ya Taa kwenye mtaa wa Qianmen mjini Beijing

    (GMT+08:00) 2009-02-09 17:03:41

    Siku kuu ya Taa imewadia, mtaa wa Qianmen utaalika makundi ya michezo ya jadi ya sehemu mbalimbali kufanya maonesho, vilevile yataoneshwa mabaki ya utamaduni usioonekana katika sherehe ya siku kuu hiyo.

    Caijie ni mtindo mwingine wa maonesho ya sanaa ya jadi ya China, unafanana na maonesho yanayofanyika katika mandamano ya nchi za nje, wachezaji huwa wanafanya maonesho huku wanakwenda mbele, na watazamaji wanatazama katika kandombili za barabara. Katika tarehe 9 mwezi Februari,watu wanaweza kuona maonesho murua ya siku kuu. Naibu mkurugenzi wa kituo cha michezo ya utamaduni na sanaa cha idara ya utamaduni ya mji wa Beijing, Zhang Wei alisema,

    "Mtaa wa Qianmen ni mtaa wenye historia ya miaka mingi, hivyo tumechagua sehemu hiyo na kufanya maonesho ya Caijie ili kukuza utamaduni wa jadi. Katika maonesho ya Caijie, itaoneshwa michezo mizuri ya ngoma na sarakasi."

    Licha ya hayo, idara ya maandalizi imejenga jukwa la michezo huko ili kuonesha michezo ya jadi ya China ya vivuli vya wanasesere waliotengenezwa kwa ngozi ya punda na michezo ya vikaragosi, kitu kinachofurahisha zaidi ni kuwa mabingwa 8, ambao ni warithi wa mabaki ya utamaduni usioonekana wa China, watafanya maonesho ya kazi za sanaa za mikono mbele ya watu. Bw. Zhang alisema,

    "Ufundi huo wa jadi halisi unarithiwa kizazi baada ya kizazi. maonesho mengine ni ya ngazi ya taifa na ya kimataifa, vilevile kuna maonesho ya picha. Watalii wanaweza kuona ufundi wa jadi unaorithiwa na mafundi wakifanya kazi mbele ya watu, zikiwa ni pamoja na vinyago vya jade, vitu vya cloisonne, kuchonga nakshi na mapambo kwenye mgando wa rangi zilizopakwa kwenye vyombo, na maua yaliyotengenezwa kwa kitambaa cha hariri."

    Katika siku kuu ya Taa, mchezo wa vitendawili wa jadi pia umefanyika katika mchezo wa Caijie, ambapo watu wanaweza kufahamu zaidi utamaduni wa jadi wa China na kuona furaha ya kushiriki.


    1 2 3
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako