Katika miaka ya 20 na 30 ya karne iliyopita, pamoja na kuingia kwa utamaduni wa nchi za magharibi, majengo yaliyojengwa yalianza kuwa na mtindo wa majengo ya magharibi kwa kiwango fulani, majengo ya kimagharibi na majengo yenye saa yanachanganyika na majengo ya jadi ya China. Bw. Li Bo alisema, ili kurejesha sura ya wakati ule, idara ya hifadhi ya vitu vya utamaduni, ilifanya marekebisha kuhuhusu majengo ya mtaa huu ikifuata kanuni ya kufanya ukarakati na kurejesha sura ya zamani ya majengo. Alisema,
"Toka mwaka 2002, tuliwaita wataalamu kumi kadhaa kufanya utafiti ili kurejesha sura ya zamani na kudumisha thamani ya kiutamaduni na kibiashara ya mtaa huu. Watalii wanaweza kuona hali ile ya miaka kumi kadhaa hata ya 100 iliyopita, kufahamu historia, utamaduni wa Beijing ya zamani na kuona hali ya ustawi ya mtaa wa Qianmen wa zamani.
Baada ya kufanyiwa ukarabati, mtaa wa Qianmen ulizinduliwa upya siku chache kabla ya kufanyika michezo ya Olimpiki mwezi Agosti mwaka uliopita, mejengo ya jadi na maduka ya miaka mingi yaliyoko kwenye mtaa huu yanatembelewa kila siku na watalii wengi wanaotoka sehemu mbalimbali za dunia. Hivi sasa mtaa wa Qianmen unakataza magari kupita isipokuwa gari maalumu linalopita kwenye njia ya reli
"mtaa wa Qianmen unadumisha kumbukumbu ya wakazi wa zamani wa Beijing, vilevile unavutia nyoyo za wakazi wa zamani wa Beijing waliohamia sehemu nyingine. Mtalii Wang Xinlu aliwatembelea marafiki zake waliokuja pamoja naye kutoka sehemu ya nje ili kuona pilikapilika za wakati ule. Alisema,
"Mabasi yaliweza kupita kwenye mtaa huu hapo zamani, maduka yalikuwa mengi moja baada ya lingine, nilikuja kucheza hapa mara kwa mara, kuna vitu vingi vya kuvutia. Sasa umebadilika na kuwa wa kupita watu tu, naona ni umaalumu mwingine wa mtaa."
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |