• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • "Azizi tatu" za Lanzhou

    (GMT+08:00) 2009-03-16 17:58:59

    Mto Manjano unaitwa mto mama wa taifa la China. Mji wa Lanzhou ulioko sehemu ya kaskazini magharibi ya China ni mji wa kwanza kwa ukubwa kwenye sehemu ya mwanzo ya mtiririko wa mto Manjano unaopita katikati ya mji huu.

    Mji wa Lanzhou ni mji mkuu wa mkoa wa Gansu, vilevile ulikuwa mji muhimu sana kwenye njia ya biashara ya hariri katika zama za kale nchini China, hivyo mji huu una mabaki mengi ya utamaduni wa mto Manjano na njia ya biashara ya hariri.

    Wimbo unaimbwa hivi: "Maji ya mto Manjano yanatiririka daima, yanapita maskani yangu Lianzhou, jamaa zangu walioko mbali wanataka niimbe wimbo wa mto Manjano………"

    Upande wa kaskazini mwa mji wa Lanzhou kuna mlima Baitai, upande wake wa kusini kuna mlima Benlan, na ile sehemu nyembamba ya kati ni mji wa Lanzhou, ambapo mto Manjano unapita katikati yake. Mji wa Lanzhou ni mahali pazuri pa kukwepa joto kwa watu katika majira ya joto.

    Hali ya hewa nzuri kutokana na umaalumu wa jografia ya huko, Lanzhou inapata mwangaza wa jua wa kutosha, na imekuwa maarufu kwa uzalishaji wa matunda na matikiti, kila ifikapo mwezi Julai na Agosti, watu wengi wanakwenda huko kukwepa joto kali na kula matunda ya huko.

    Watu wa Lanzhou walisifu mji huo wakisema, "Maji ya mto Manjano yanatiririka daima, samaki wanaogelea katika maji kwa furaha. Vyombo vya kuchotea maji vya kizamani vinafanya kazi bila kusita, mandhari ya asili ya hapa ni ya kupendeza. Jina la Lanzhou linavuma kutokana na wingi wa utamu wa matunda."


    1 2 3
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako