Pamoja na mandhari nzuri ya asili ya Lanzhou, vitu vitatu vinavyopendwa sana na wakazi wa huko ni mto Manjano, jarida la "Wasomaji" na tambi zenye nyama ya ng'ombe ya Lanzhou.
Mto Manjano ni muhimu sana kwa Lanzhou kama mshipa mkuu wa mji. Chelezo cha ngozi ya kondoo(sheepskin rafts), chombo cha kuchotea maji kwa nguvu za upepo kwenye mto Manjano na daraja la chuma la mto Manjano ni vitu muhimu vya utamaduni maalumu wa mto Manjano, ambavyo vilikuwa muhimu sana katika maisha ya watu.
Hapo zamani hakukuwa na daraja kwenye mto Manjano wa sehemu ya Lanzhou. Wakazi wa huko walitumia njia ya asili ya kuvuka mto na kusafirisha vitu kwa vyelezo vya ngozi ya kondoo katika miaka elfu kadhaa iliyopita.
Mkurugenzi wa idara ya utamaduni na uchapishaji ya mji wa Lanzhou, Bw. Fan Wen alisema:
"Vyelezo vya ngozi ya kondoo vilifanya kazi muhimu zaidi katika uenezi wa utamaduni kuliko kazi za usafirishaji. Mji wa Lanzhou uko kwenye sehemu ya mwanzo ya mto Manjano, ambako ni mahali wanapokaa kwa wingi watu wa makabila mengi. Uvumbuzi na utengenezaji wa vyelezo vya ngozi ya kondoo ilianza kuunganisha utamaduni wa makabila mbalimbali. Mwishoni mwa miaka ya 50 na mwanzoni mwa miaka ya 60, zana nyingi za kikazi zilisafirishwa huko kwa kutumia vyelezo vya ngozi ya kondoo. Kwa mfano, wakati kilipojengwa kiwanda kwenye sehemu ya Qingtongxia mkoani Ningxia, zana za kikazi zenye uzito wa tani 20 hadi 30 hivi zilishindwa kupelekwa huko, kwani wakati ule kulikuwa hakuna njia ya reli katika sehemu ya Qingtongxia. Kwa hiyo, zana zile zilisafirishwa kwanza hadi mji wa Lanzhou, halafu zilisafirishwa tena hadi huko kwa vyelezo vya ngozi ya kondoo.
Utamaduni wa mto Manjano ni mkubwa sana, licha ya vyombo vya mawasiliano na uzalishaji mali vikiwemo vyelezo vya ngozi ya kondoo na chombo cha kuchotea maji, ambavyo vilivumbuliwa kutokana na akili za watu, jarida la "Wasomaji" ni lenye utamaduni zaidi na athari kubwa ndani na nje ya China, ambalo lilianza kuchapishwa zaidi ya miaka 20 iliyopita.
Mhariri mkuu pamoja na wanafunzi kadhaa wa vyuo vikuu walianzisha shirika la jarida la "Wasomaji" miaka 27 iliyopita, ambapo mwanzoni yalitolewa majarida elfu 30 tu, lakini baada ya miaka 3, yalianza kuchapishwa majarida laki 5 katika kila toleo, na kuvunja rekodi ya ongezeko kwa majarida ya nchini China. Sasa miaka 27 imepita, jarida hilo linachukua nafasi ya kwanza miongoni mwa zaidi ya aina 9,000 za majarida za nchini China. Hivi leo, jarida la "Wasomaji" siyo jarida maarufu tu, bali ni lenye mambo mengi ya utamadunia wa mji, na kuwa alama ya mji wa Lanzhou.
Kudumisha ubora wake katika miaka 20 iliyopita, kumefanya jina la jarida hilo kuvuma siku hadi siku. Mhariri mkuu wa jarida hili, Bw. Peng Changcheng alisema,
"Baada ya jarida hili kuingia katika karne ya 21, tulitoa wito wa kulifanya jarida hilo kuwa kitabu cha roho cha Wachina. Tunaendelea kudumisha mtazamo wa ufunguaji mlango na ufuatiliaji wa hisia za watu."
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |