• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • "Azizi tatu" za Lanzhou

    (GMT+08:00) 2009-03-16 17:58:59

    Chakula kinachopendwa zaidi na watu wa Lanzhou ni tambi zilizotengenezwa kwa kuvutwa na mikono na kutiwa katika supu ya nyama ya ng'ombe. Wenyeji wa Lanzhou wanapenda kula tambi, hususan tambi zilizotengenezwa kwa kuvutwa na mikono na kutiwa katika supu ya nyama ya ng'ombe. Hivi sasa tambi za aina hiyo zimepata sifa kubwa na kupatikana katika sehemu mbalimbali za China. Katika Lanzhou, tambi zenye nyama ya ng'ombe zinachukua nafasi ya kwanza katika chakula cha haraka. Wenyeji wa Lanzhou wanasema, wanaona wasiwasi kama wasipokula tambi zenye nyama ya ng'ombe kwa siku 3.

    Wengine walisema, "katika baadhi ya nyakati, nikirudi kutoka safarini, mimi huenda mkahawa unaouza tambi zenye nyama ya ng'ombe kabla ya kufika nyumbani!"

    Tambi zenye nyama ya ng'ombe za Lanzhou zimekuwa na historia ya zaidi ya miaka 90, mwislam Bw. Ma Baozi wa Lanzhou ndiye mtu aliyeanzisha tambi za aina hiyo. Hivi sasa mrithi wa chakula hicho, mtoto wa binti yake, Bw. Sun Haichang amevumbua mapishi mapya na mazuri zaidi yanayoambatana na matakwa ya watu wa sasa. Hivi sasa, tambi zenye nyama ya ng'ombe si aina ya chakula cha haraka tu, bali zimekuwa aina ya utamaduni wa chakula.


    1 2 3
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako