• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bonde kubwa la Nujiang mkoani Yunnan

    (GMT+08:00) 2009-04-06 20:30:50

    Mto Nujiang ni mkubwa ulioko sehemu ya kusini magharibi ya China ya mkoa wa Yunnan, ambao ni moja ya maeneo yanayopita Mto Nujiang, ni eneo muhimu wanapoishi watu wa makabila madogo madogo nchini China.

    Wimbo unaosikia sasa hivi ni wimbo unaoimbwa na Walili kwa lugha ya kabila lao, wimbo huu unaimbwa na mwenyeji wakati wa kuwakaribisha wageni pombe. Maskani ya Walili yako kwenye wilaya ya Nujiang iliyoko sehemu ya kaskazini magharibi ya mkoa wa Yunnan. Licha ya kabila la Walili, sehemu hiyo pia ni mahali wanapoishi watu wa makabila ya wanu, wadulong, wahan, wapumi, wayi, watibet na waDai, na jumla ya idadi ya watu wa makabila madogo ni zaidi ya 90%.

    Eneo la wilaya ya Nujiang ni kiasi cha kilomita 14,000, ambalo sehemu ya kaskazini ina mwinuko na sehemu ya kusini imeinama chini. Eneo hilo lote ni milima mikubwa na mito, ambayo ni pamoja na mito Nujiang, Lancangjiang na Dulongjiang. Hivyo watu hawafahamu vizuri vivutio vya bonde kubwa la Nujiang. Mkazi wa huko, Bw. Chen Jun alitufahamisha kuhusu maskani yao.

    "Mandhari ya maskani yetu ni nzuri sana, watu wa kwetu hapa pia ni wema na wakarimu; uzuri wa hapa ni wa kimaumbile, wala siyo ya kutengenezwa na watu."

    Mfanyakazi wa idara ya utalii ya wilaya ya Nujiang, Bw. Zhao Wensheng alisema,

    Bonde zima la Mto Nujiang ni kama kitabu kizito cha falsafa kuhusu utamaduni na mazingira ya asili, ukitembelea hapa unaweza kujihisi mengi.


    1 2 3
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako