Popote mtalii anapofika, maji ya Mto Nujiang yanamfuata kama kivuli chake. Baada ya kufika sehemu ya mwanzo ya Mto Nujiang, maji ya mto yanabadilika sana: maji mengi ya mto yanapofika tarafa ya Bingzhongluo kutoka bonde la Qiunatong lililoko upande wa kaskazini wa Mto Nujiang, yanapita upande wa kusini wa tarafa hiyo hadi kufika tarafa ya Dala, kutokana na kuzuiliwa mara nyingi na mawe ya milima, Mto Nujiang unazunguka kwa nusu duara, hivyo sehemu hiyo inaitwa "nusu duara ya kwanza ya Mto Nujiang". Katika majira ya joto na kupukutika majani, maji ya Mto Nujiang huwa ni mengi na yanatiririka kwa kasi; katika majira ya baridi na Spring, maji ya mto ni maangavu sana. Mfanyakazi wa sehemu hii yenye mandhari nzuri, Bw. Li Wanlin alisema,
"Umaalumu wa 'nusu duara ya kwanza ya Mto Nujiang' ni kuwa mto unapinda sana kwenye sehemu hiyo, ambapo ardhi ya upande wa ndani inaonekana kama kisiwa. Wakati wa asubuhi, kijiji na nyumba za wakazi zinaonekana kidogo na katika wakati mwengine hazionekani kabisa kutokana na kufunikwa na ukungu."
Katika upande wa kaskazini wa tarafa ya Bingzhongluo, mlima wa Gaoligong na mlima wenye theluji wa Biluo, ambayo Mto Nujiang unapita kati kati yao, inakutana huko. Magenge mawili yenye urefu wa zaidi ya mita 500, yanaonekana kama lango kubwa la mawe lenye upana karibu mita 200. Wenyeji wa huko wanaliita kuwa "nayiqiang" yaani lango ambalo hata majini wanashindwa kulipita. Bw. Li Wanlin alisema,
"Lango la mawe ni kubwa ajabu, ambalo ni magenge yenye urefu wa kwenda juu mita 500. Kulitazama kutoka mbali linaonekana ni mlango kabisa, ambapo ni njia moja muhimu ya kuingia Tibet."
Tarafa ya Bingzhongluo ni mahali penye vivutio vingi vya kimaumbile kwenye sehemu ya Nujiang, na inasifiwa kama ni pahali pazuri kabisa wanapokaa kwa pamoja binadamu na miungu. Mbele ya milima yenye theluji isiyoyeyuka katika majira yote ya mwaka, ni mashamba safi yenye mazao ya kilimo, yenye rangi za manjano na kijani, pamoja na nyumba za wakulima za rangi ya kijivu kizito, ambazo moshi wa kupika chakula unatapakaa angani, sehemu hii ni shwari na yenye mandhari ya kupendeza ya shambani. Watu wengi walifika huko kwa ajili ya kutaka kukwepa adha ya mijini na kujiburudisha kwa hali ya shwari ya mazingira ya asili. Mtalii mmoja kutoka mkoa wa Guangdong alifika Bingzhongluo zaidi ya miaka 10 iliyopita, ambaye alieleza uchangamfu na urafiki wa wakazi wa huko kwenye mtandao wa Inter-net, tokea hapo idadi ya wageni wanaofika huko inaongezeka kila siku ipitayo, wakiwemo wageni wa nchi zaidi ya 10.
Wenyeji wa huko wanaleta pombe na kuimba nyimbo za kuwakaribisha wageni.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |