• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bonde kubwa la Nujiang mkoani Yunnan

    (GMT+08:00) 2009-04-06 20:30:50

    Kivutio kikubwa zaidi kwenye bonde la Nujiang ni Shiyueliang, ambao ni "mwezi wa nawe" katika lugha ya Kichina. Kutazama kutoka mbali, kati ya milima, kuna tundu moja kubwa la mawe linaloonekana kama mwezi mpevu ulioko angani, kupitia tundu hilo, watu wanaweza kuona mawingu yaliyoko nyuma yake. Katika miaka ya 30 ya karne iliyopita, kipindi cha kupambana na mashambulizi ya Japan, jenarali C. L. Chennault pamoja na marubani wa ndege aliowaongoza, waliachana na uelekezaji njia wa ardhini, walichukulia mandhari hiyo maalumu ya kijografia kuwa alama muhimu ya ardhini ya kujua upande wanaokwenda. Kivutio cha mwezi wa mawe kimekuwa na maana isiyo ya kawaida kutokana na historia hiyo ya urafiki wa China na Marekani.

    Mto Nujiang wenye urefu wa zaidi ya kilomita 3,200 unaanzia upande wa kusini wa mlima wa Tanggula, maji yake yanaingia ghuba ya Bangladesh mwishoni baada ya kupita kwenye mkoa unaojiendesha wa Tibet, mkoa wa Yunnan na Myanmar. Katika majira ya baridi, maji ya Mto Nujiang yanatiririka kwa taratibu kwenye bonde kubwa la Nujiang, ila tu yanapofikia mahali panapoitwa "Laohutiao", maana yake katika lugha ya Kichina ni "mruko wa chui mkubwa"(tiger), maji ya mto yanaonekana kama yanaanguka kutoka angani. Watu wanasikia ngurumo kali na kuona mawimbi makubwa.

    Kuna hadithi moja nzuri kuhusu kivutio cha "mruko wa chui mkubwa", inasemekana kuwa mwana wa mfalme alibadilishwa kuwa chui mkubwa na mchawi bi kizee, chui mkubwa alipomuwaza mchumba wake mzuri, alirukia kwenye kando ya mto anakokaa msichana yule. Udhati wa moyo wake ulimvutia mungu, chui mkubwa akabadilika tena kuwa bin mfalme, kisha walifunga ndoa.

    Hapo zamani, hakukuwa na daraja kwenye Mto Nujiang, ambapo watu walivuka mto kwa kutumia mnyororo mkubwa wa chuma uliofungwa kwenye kando mbili za mto. Hivi sasa kuna madaraja mengi yanayotundikwa kwenye mto na madaraja yanayojengwa juu ya minyororo ya chuma. Wakazi wa kando mbili za Mto Nujiang, ambao waliwasiliana kwa kutumia mnyororo wa chuma uliofungwa juu ya mto kizazi hadi kizazi, sasa wanatumia chombo hicho cha kuvuka mto chenye kutisha na kuchangamsha kuwa kama mchezo wa utalii. Ikiwa wewe ni jasiri, unaweza kuujaribu. Bi. Liu kutoka Beijing, alisema kwa furaha:

    "Nilipofunga mkanda wa usalama, nilikuwa na hofu kidogo, lakini baada ya kuteleza kwenye umbali wa mita zaidi ya 10, sikuogopa tena, ninaona inanichangamsha sana, ninafurahia safari ya kuja hapa."


    1 2 3
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako