• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jumba la makumbusho la Magenge Matatu

    (GMT+08:00) 2009-04-20 16:30:48

    Sehemu ya Magenge Matatu ni moja kati ya sehemu muhimu zinazopita Mto Changjiang, na mji wa Chongqing ulioko sehemu ya kusini magharibi ya China ni mji muhimu sana kwenye sehemu hiyo. Sasa tunapenda kuwafahamisha Jumba la makumbusho la Magenge Matatu la mji wa Chongqing pamoja na historia, utamaduni na msingi wa mambo ya utamaduni wa mji huu na sehemu ya Magenge Matatu.

    Jumba la makumbusho la Magenge Matatu linachukua nafasi ya kwanza kwa ukubwa wake kati ya majumba ya makumbusho ya vitu maalumu mbalimbali, ambalo ni moja kati ya "majengo kumi maarufu ya Asia katika karne ya 20". Jumba hilo la makumbusho liko kwenye kando ya uwanja wa umma, na kutazamana na Jumba la mikutano ya umma la Chongqing. Jumba la makumbusho lenye mita za mraba zaidi ya elfu 40, lilijengwa mwaka 2005, eneo la kumbi za maonesho za jengo hilo ni kiasi cha mita za mraba elfu 23. Jengo hilo lilijengwa kwa kuzingatia wazo la ubunifu wa boma kubwa la bwawa la Magenge Matatu, ujia mkubwa wa udhibiti wa mazingira ya asili uliojengwa kwa kioo chenye umbo la tao kwenye lango la jengo, unaonekana kama maporomoko ya maji, jinsi ilivyo ni ya kupendeza sana.

    Vitu vinavyohifadhiwa kwenye jumba la makumbusho hivi sasa ni zaidi ya laki 1.7, ambavyo vinaoneshwa kwenye sehemu nne. Naibu mkuu wa jumba la makumbusho, Bw. Liu Chunming alisema, vitu hivyo vinaonesha chimbuko la historia ya Magenge Matatu na mji wa Chongqing. Alisema:

    "Ukumbi wa kwanza ni kuhusu Magenge Matatu, watu wanaweza kuona hali ya maumbile, jografia, utamaduni, na ujenzi wa mradi wa Magenge Matatu. Ukumbi wa pili ni kuhusu historia ya Magenge Matatu na sehemu za Ba na Yu za kabla ya enzi ya Han. Ukumbi wa tatu ni kuhusu historia ya mji wa Chongqing katika miaka ya karibuni. Ukumbi wa nne ni kuhusu historia ya miaka ile ya kupambana na mashambulizi ya Japan."


    1 2 3
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako