Habari zinasema, licha vitu vya kiutamaduni vilivyofukuliwa chini ya ardhi, vitu 246 vya kiutamaduni vilivyoko juu ya ardhi, vikiwemo Baiheliang, hekalu la Zhang Fei na kijiji cha Shibao, pia vimehifadhiwa vizuri. Baiheliang ni jiwe kubwa lenye urefu wa kiasi cha mita 1,600 na upana wa mita 16. Jiwe hilo linaonekana katika majira ya baridi tu, ambapo maji ya mto huwa ni machache, lakini msimu wa mvua jiwe hilo kubwa hufunikwa kabisa na maji, shirika la elimu, sayansi na utamaduni la Umoja wa Mataifa lilisifu jiwe hilo kuwa ni "kituo cha uchunguzi wa hali ya mto cha kale kilichohifadhiwa vizuri na cha kipekee duniani". Bw. Wang Ping alisema, baada ya kufanya ukarabati, watalii wataweza kuona uzuri wake katika siku chache zijazo. Alisema:
"Baiheliang itafunguliwa kwa watalii mwezi Mei mwaka huu, huu ni mradi wa kuhifadhi vitu vya mabaki ya kale ya utamaduni kwa teknolojia za aina kadhaa. Jiwe hilo lilikuwepo chini ya maji, sasa tunaendelea kufanya jiwe hilo liwe chini ya maji, hapo zamani ni katika majira ya Spring tu, ambapo maji ya mto huwa machache, watu wanaweza kuliona, lakini katika siku za baadaye watu wataweza kuliona katika wakati wowote, zaidi ya hayo, mbinu zinazotumika katika maonesho pia ni za kisasa. Hakalu la Zhang Fei lililohamishwa kwenye sehemu mpya, sasa limefikia hatua ya kufunguliwa kwa watalii vilevile."
Ukumbi kuhusu "njia ya maendeleo ya mji wa Chongqing" unapendwa zaidi na wakazi wa miaka mingi wa Chongqing. Barabara iliyojengwa kwa mawe yenye rangi ya kijivu, ghorofa zenye pembe za mapaa zilizoinuka juu, duka la kinyozi na mkahawa wa chai, vinaonekana kwenye kielelezo cha barabara, watazamaji wanaona wamerudi katika nyakati zile za zamani. Katika ukumbi wa mwisho, watu wanaweza kuona ushujaa wa mji wa Chongqing katika miaka ya mapigano dhidi ya mashambulizi ya kijapani.
Jumba la makunbusho la Magenge Matatu ni kama kitabu kikubwa cha historia cha sehemu hiyo, na lilikuwa wazi kwa watu wote tangu tarehe 26, mwezi Machi mwaka 2008
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |