Magenge Matatu ni kama njia ya ustaarabu na historia ya taifa la China, ambayo inapamba milima na mito ya sehemu ya Ba(mji wa Chengdu kwa sasa) na sehemu ya Shu(mkoa wa Sichuan kwa sasa), vilevile ni njia ya ustaarabu inayounganisha ustaarabu wa sehemu ya kusini magharibi na sehemu ya mashariki za China. Katika ukumbi kuhusu Magenge Matatu, ustaarabu wa mto Changjiang umeoneshwa vilivyo hapo.
Vitu vingi vinavyooneshwa kwenye ukumbi huu ni pamoja na vitu maalumu vya utamaduni vya sehemu hiyo, ambavyo vilifunikwa chini ya maji, wakati bwawa la maji la Magenge Matatu lilipolimbikiza maji. Kiongozi wa kikundi cha hifadhi na utafiti wa vitu vya utamaduni vya Magenge Matatu cha mji wa Chongqing, Bw. Wang Chuanping alisema,
"Katika ukumbi wa Magenge Matatu, watu wanaweza kuona mazingira ya kutegemeana kwa viumbe, pamoja na uhusiano maalumu kati ya binadamu na maumbile. Kwa mfano, mawe yenye alama zilizokatwa kwa kamba, ambazo wafanyakazi walitembea kando ya mto huku wakivuta kwa kamba mashua ya mizigo ya mtoni. Alama hizo zilizokatwa kwa kamba za kuvuta mashua za wafanyakazi katika miaka zaidi ya 1,000 iliyopita zinaonesha uhusiano wa maisha ya wafanyakazi waliovuta mashua na mazingira ya maumbile. Kwa hiyo, mtu anaweza kuona alama zilizobaki kutokana na kukatwa na maji ya mtoni katika miaka mingi iliyopita, pamoja na muundo wa kijiolojikol wa ardhi kwenye milima iliyoko kando mbili za mto, mawe yote hayo yanawashangaza sana watazamaji. "
Ukumbi wa jirani ni ukumbi wa maonesho kuhusu Ba, Yu za zamani za kale(miji ya Chengdu na Congqing kwa sasa), vitu vyote vinavyooneshwa kwenye ukumbi huu ni vitu visivyo vya kawaida. Bw. Wang Chuanping alisema, sehemu ya bwawa la Magenge Matatu ina rasilimali kubwa ya kiutamaduni, ambayo ilihimiza uhifadhi wa haraka wa vitu vya mabaki ya kale ya utamaduni ya sehemu hiyo. Alisema:
"Katika zaidi ya miaka 10 iliyopita, tulifukua vitu vya mabaki ya kiutamaduni kwenye mita za mraba milioni 1.3, kama hakuna ujenzi wa mradi wa Magenge Matatu, kazi hizo zingemalizwa katika muda mrefu wa vizazi kadhaa. Lakini kutokana na mradi huo, tulitumia muda wa zaidi ya miaka 10, sisi tulifukua vitu vya mabaki ya kale ya utamaduni vya kale laki 1.5, ambavyo zaidi ya elfu 10 ni vyenye thamani kubwa. Kwa mfano, mawe yenye maneno ya kumbukumbu ya makaburi ya enzi ya Han ni nadra sana kuonekana katika China. Kutokana na shughuli hizo, tumefahamu kuwa sehemu ya Magenge Matatu ni makazi ya asili ya binadamu katika mashariki ya dunia."
Wang Chuanping alisema, kikundi cha uhifadhi na utafiti wa mabaki ya utamaduni kinafanya utafiti kuhusu maendeleo ya binadamu kwenye sehemu ya Magenge Matatu. Sasa wamefahamu zaidi kuhusu vitu vilivyotumiwa na watu wa kale walioishi kwenye sehemu ya Ba, jambo ambalo linasaidia sana utafiti kuhusu chanzo na maendeleo ya wakazi wa zamani za kale kwenye sehemu hiyo, uanzishaji wa nchi ya Ba na namna wakazi wa Ba walivyojiunga na kabila la Wahan.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |