• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Maua ya camellia ya Dali, Yunnan

    (GMT+08:00) 2009-04-27 19:15:47

    Maua ya camellia ni maua maarufu ya jadi ya China, na ni moja ya maua maarufu katika dunia. Umbo la ua la camellia ni zuri sana, rangi na majani ya maua hayo ni ya kuvutia, hivyo maua ya camellia yanathaminiwa sana katika mabustani ya dunia nzima. Sasa tunawafahamisha maua ya camellia ya jimbo linalojiendesha la kabila la Wabai la Dali, mkoani Yunnan.

    Dali iko upande wa magharibi wa sehemu ya kati ya mkoa wa Yunnan na kusini mwa Milima Henduan, huko kuna aina nyingi zaidi za maua. Watu husema, ukifika Yunnan usikubali kukosa kuangalia maua ya camellia. Maua ya camellia ya Dali ni mazuri zaidi katika mkoa wa Yunnan. Data za historia zinasema, maua ya camellia yalianza kupandwa kwa wingi huko Dali katika enzi za Tang na Song (mwaka 649 hadi mwaka 902), na yanapandwa kwenye bustani ya mfalme yakichukuliwa kama ua la kitaifa na jamaa za mfalme na mawaziri.

    Katika karne ya 17, waingereza waliingiza maua ya camellia ya Dali nchini mwao, na kuyapanda katika bustani ya kasri ya Buckingham. Baadaye, maua ya camellia yalipendwa na watu wa nchi mbalimbali za Ulaya kutokana na maua yake kuwa makubwa, rangi maridadi, harufu nzuri na kuonekana kuwa ni ya hali ya juu. Muda si muda, nchi nyingi za bara la Amerika na bara la Asia ziliingiza maua ya camellia na kuyapanda katika nchi zao.

    Dali ikiwa ni chimbuko la asili la maua ya camellia ya Yunnan, sasa imekuwa sehemu muhimu ya uzalishaji wa maua ya camellia na kuwa na camellia za aina bora za asili kadha wa kadha. Habari zinasema, katika sehemu ya Dali yanaota maua mengi ya camellia mwitu, ambayo idadi ya miti mikubwa imezidi elfu 50. Mbali na hayo Dali ina mti mmoja wa maua ya camellia wenye kimo cha zaidi ya mita 17, ambao uliota zaidi ya miaka 400 iliyopita, mti huo wa maua una kimo kikubwa zaidi kuliko miti yote ya maua ya camellia ya duniani. Mkuu wa jumuiya ya maua ya camellia ya mji wa Dali, Zhang Jianchun alisema, kuweko rasilimali kubwa ya maua ya camellia kunatokana na mazingira maalumu ya kimaumbile na kijografia ya sehemu ya Dali. Alisema:

    "Chimbuko la asili kabisa kwa maua ya camellia ni kwenye sehemu yenye mwinuko wa mita 2,600 hadi mita 2,800 ya Mlima Cang na Mlima Galigong. Mazingira ya kipekee ya asili ya Dali yamewezesha aina nyingi za viumbe, maua ya camellia na maua ya azalea ambayo ni aina maalumu za maua ziote huko Dali. Kwa mfano aina 8 maarufu za maua ya camellia ya Yunnan, zote zinaoteshwa huko Dali, kuna msemo mmoja unaosema, maua ya camellia ya Yunnan yanachukua nafasi ya kwanza duniani, na maua ya camellia ya Dali yanachukua nafasi ya kwanza katika mkoa wa Yunnan."

    Katika miaka mingi iliyopita, wakazi wa Dali walipenda maua ya camellia, hivyo maua ya camellia yana msingi mkubwa wa kiutamaduni. Katika mji wa kale wa Dali, kote kuna miti ya camellia iliyoota zaidi ya miaka 100 iliyopita. Karibu katika kila ua wa nyumba ya wakazi wa huko mtu anaweza kuona miti ya maua ya camellia.


    1 2 3
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako