• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Maua ya camellia ya Dali, Yunnan

    (GMT+08:00) 2009-04-27 19:15:47

    Toka mwaka 2008, Dali imeanzisha shughuli nyingi kubwa zinazohusiana na mtaa wa camellia wa China, ikiwa ni pamoja na "Maonesho ya kimataifa ya orchid na camellia ya Dali, China, ambayo yanafanyika kila mwaka. Shighuli hizo zimefanya maua ya Dali kuwa na sifa nzuri, ambayo imethibitishwa na wataalamu wa sekta ya maua akiwemo mwenyekiti wa jumuiya ya kimataifa ya camellia, Bw. Gregory Davis, na kufanya Dali kupewa kibali cha kuandaa mkutano wa camellia wa dunia wa mwaka 2016. Naibu mwenyekiti wa kanda ya China wa jumuiya ya camellia ya kimataifa, Bw. You Muxian alipongeza ufanisi wa shughuli hizo, akisema,

    "Nimefika Dali mara 5. Ninaona maonesho ya camellia ya mwaka huu ni mazuri zaidi kuliko yale ya mwaka uliopita, hususan kuwa na maua mengi na ya aina yingi zaidi ikilinganishwa na mwaka uliopita. Hasa ni kufanya maonesho ya maua 1,000 ya camellia, ambayo yanalingana na maonesho ya kimataifa."

    Habari zinasema, Dali ikiwa ni moja kati ya sehemu maarufu za utalii na maeneo wanayokaa kwa wingi watu wa makabila madogo mkoani Yunnan, Dali imefungamanisha maua na shughuli za utalii za huko. Kwa mfano Dali inafanya tamasha kwenye mtaa wa camellia katika muda wa sherehe za siku kuu ya jadi ya "Sanyuejie". Mkuu wa jumuiya ya camellia ya mji wa Dali, Bw. Zhang Jianchun alisema,

    "Maonesho ya camellia kwenye mtaa wa camellia ni shughuli muhimu katika sherehe za siku kuu ya "Sanyuejie". Maua yanayooneshwa kwenye mtaa huo mwaka huu ni ya aina 136, maua yanaoneshwa kwenye sehemu tatu, maua ya sehemu ya kwanza ni camellia za hapahapa Dali, sehemu ya pili ni camellia zilizoagizwa kutoka nchi za Marekani, Australia na New Zealand, na sehemu ya tatu ni maua ya camellia ya mikoa ya Jiangsu na Zhejiang ya China. Kwa jumla, maonesho ya mtaa wa maua ya camellia ya mwaka huu yamekuwa matembezi maalumu ya utalii na kutoa huduma ya kununua camellia katika sherehe za siku kuu ya "Sanyuejie".


    1 2 3
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako