Kuna mifano mingi kuhusu athari za maua ya camellia kwa maisha ya wakazi wa huko. Michoro na mapambo mengi ya nyumba za wenyeji wa huko ni kuhusu maua ya camellia. Nguo za watu wa kabila la Wabai hazikosi mapambo yenye michoro ya camellia, hata msichana mzuri anapenda kupewa jina la "Ua la Dhahabu", hii inaonesha hadhi maalumu ya camellia nyoyoni mwa wenyeji wa Dali.
Ili kuongeza sifa za alama ya camellia duniani na kuanzisha soko maalumu la maua ya cemellia, jimbo la Dali limejenga mtaa wa camellia wa China katika mji wa Dali wenye eneo la kiasi cha mita za mraba elfu 12. Soko hilo lilifunguliwa mwanzoni mwa mwaka 2007, hivi sasa kuna maduka zaidi ya 30 ya maua, miti ya maua ya camellia zaidi ya aina 180 inayouzwa kwenye soko hilo ni zaidi ya elfu 80, na pato lake ni zaidi ya Yuan milioni 100 kwa mwaka.
Habari zinasema, umaalumu wa mtaa wa camellia wa China ni kufanya maonesho na uuzaji wa maua kwa pamoja. Licha ya hayo mtaa wa camellia unahimiza uuzaji wa maua kwa kufanya maonesha maalumu ya maua na kuuza maua kwenye mtandao wa Inter-net. Zhang Ruirong ni mfanya-biashara mkubwa wa maua kwenye mtaa wa camellia, alisema, soko hilo linawanufaisha wanunuzi na wafanya-biashara kwa pamoja. Alisema:
"Tangu kuanzishwa kwa shughuli za mtaa wa camellia wa China za kuyafanya maua ya camellia kuingia majumbani mwa watu miaka miwili iliyopita, sasa nina zaidi ya miti elfu 20 ya maua ya aina nne maarufu, hivi sasa biashara yangu inachukua nafasi ya kwanza hapa Dali kwa hivi sasa. Bei ya maua ya camellia ilikuwa ya juu kidogo katika miaka ya nyuma, baada ya jimbo la Dali kufanya maonesho ya biashara ya maua ya cemellia mwaka huu, maua ya camellia yanauzwa vizuri sana, tena bei yake ya hivi sasa inafurahiwa na watu wa kawaida, ambapo kila familia ina uwezo wa kununua na kupanda miti ya camellia. Biashara yangu ni nzuri sana, mwaka huu miti ya maua imenunuliwa na wafanya-biashara waliotoka wilaya na miji ya karibu."
Mbali na wafanya-biashara wa maua waliofika huko kununua maua kutoka sehemu nyingine, wakazi wa kawaida wa hukohuko Dali pia ni moja ya makundi muhimu ya wanunuzi. Mkazi mmoja wa mji wa Dali aliyekwenda huko kununua maua, alisema,
"Ninafika hapa kutaka kujua bei ya maua ya hivi sasa. Kama ni bei nzuri, nitanunua aina moja au mbili za miti ya maua kwani wazee wa nyumbani kwangu wanapenda maua hayo. Maua hayo yameoteshwa vizuri sana, wazee wa nyumbani kwangu wote ni mabingwa wa maua, na maua mazuri yanaburudisha watu."
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |