• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mwalimu Shao Chunliang na wanafunzi wake wa makabila madogo madogo

    (GMT+08:00) 2009-05-27 16:12:35

    Kila asubuhi Bw. Shao anakwenda kwenye darasa la wanafunzi wa makabila madogo madogo, na kuwapasha habari muhimu zinazotokea kila siku, ili wafahamu vizuri mambo ya nchini China na nchi za nje. Mwaka jana aliwaambia wanafunzi wake habari ya tetemeko kubwa la ardhi lililotokea mkoani Sichuan, huku akitokwa na machozi darasani. Mwanafunzi kutoka kabila la Warussia Wu Jiakung alisema, "Mwalimu Shao alituelezea kuwa baadhi ya wanafunzi wa sehemu zilizokumbwa na tetemeko la ardhi waliwaokoa watu wengine bila ya kujijali. Wakati mwalimu Shao alipotokwa na machozi, wengi wetu pia tulilia. Baadaye alisema watu wanapaswa kusaidiana bila kujali makabila yao."

    Licha ya kuwa mwalimu wa darasa maalumu kwa wanafunzi wa makabila madogo madogo wanaojiunga na chuo kikuu, Bw. Shao pia aliwafundisha wanafunzi wa chuo cha mawasiliano ya simu cha Chuo Kikuu cha Ufundi Anuwai cha Dalian. Alisema wanafunzi kutoka makabila madogo madogo ni wepesi sana, hivyo wanapaswa kupata elimu nzuri, na ana furaha kubwa kwa kuwa pamoja na wanafunzi hao. Mara kwa mara Bw. Shao alisema kuwafundisha wanafunzi hao kwa bidii ni jambo la kawaida, na anataka kuwafundisha vizuri zaidi Alisema, "Nina uwezo wa kufanya jambo hilo, hivyo nataka kulifanya vizuri kadiri niwezavyo. Naona kuwa katika maisha mtu akiweza kufanya vizuri jambo moja hata kama liwe jambo dogo, atakuwa na furaha wakati atakapolikumbuka maishani mwake."


    1 2 3
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako