Bw. Wang Qitai ni rafiki mkubwa wa Bw. Shao, alimsifu sana kwa juhudi zake za kuwafundisha wanafunzi wa makabila madogo madogo kwa muda mrefu, alisema, "Kuna walimu wachache tu ambao wanaweza kuwatendea vizuri wanafunzi kama anavyofanya mwalimu Shao. Na amefanya hivyo kwa miaka zaidi ya 20. Kweli yeye ni mtu anayewajibika, na kufanya kazi kwa bidii toka mwanzoni hadi mwoshoni."
Mkurugenzi wa kamati ya maendeleo ya makao makuu ya utafiti wa utamaduni wa makabila madogo madogo ya sehemu za kaskazini mwa China Bw. Aixinjueluo Dechong alisema, "Mwalimu Shao alisema kitu muhimu cha kuwafundisha wanafunzi wa makabila madogo madogo ni upendo. Anawachukulia wanafunzi hao kama watoto wake, na kuwapenda kama baba yao, kwa upande mwingine pia amepata mapenzi makubwa kutoka kwa wanafunzi hao. Bw. Shao pia anawajibika sana kwa kazi yake ya elimu, na anaunganisha kazi yake na ustawi na maendeleo ya sehemu za makabila madogo madogo."
Hadi sasa idadi ya wanafunzi wa makabila madogo madogo aliowahi kuwafundisha imezidi 600, na sasa wamekuwa wataalamu, mafundi, walimu, watumishi wa serikali na wanaviwanda, na wanajenga nyumba zao kwa busara na jasho lao, ambapo Bw. Shao bado anaendelea na kazi yake ya kufundisha. Alisema hataiacha kazi hiyo mpaka ashindwe kabisa kufanya hivyo wakati atakapo zeeka sana.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |