• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kuangalia maua malus huko Huailai, mkoani Hebei

    (GMT+08:00) 2009-06-01 16:37:52

    Wakati majira ya joto yanapoingia baada ya majira ya Spring, maua malus huchanua vizuri kwenye wilaya ya Huailai, mkoa wa Hebei, China. Hivi karibuni tamasha la maua malus lilifanyika kwenye pwani ya mji wa zamani wa mji mdogo wa kale Xiaonanxinbao wilayani Huailai. Wageni kutoka sehemu mbalimbali walikwenda huko kuangalia maua hayo, kupiga picha na kuchora michoro ya maua malus. Mtalii kutoka mkoa wa Shanxi, Bw. Zhang Qingyun alimwambia mwandishi wetu wa habari akisema

    "Nimefurahi sana kupata fursa ya kushiriki kwenye tamasha la maua malus, nimeburudishwa sana na maua malus mengi."

    Mji mdogo wa kale wa Xiaonanxinbao uko kwenye sehemu ya kusini mashariki ya wilaya ya Huailai, na uko karibu na bwawa la Guanting kwa upande wa kaskazini, upande wake wa kusini ni milima Yansha, tena uko karibu na mji wa Beijing. Hali ya hewa ya sehemu hiyo ni tofauti na sehemu nyingine, hivyo inatoa mazao mengi ya kilimo, hususan inafaa sana kuota kwa miti ya malus yenye pembe nane. Katibu wa Kamati ya chama cha Kikomunisti cha China ya Xiaonanxinbao Bw. Han Zhiming alisema, miti ya malus ya aina hiyo ilianza kupandwa tangu miaka 600 iliyopita, hivi sasa sehemu hii inachukua nafasi ya kwanza nchini China kwa utoaji miti ya malus yenye pembe nane. Alisema,

    "Eneo linalopandwa miti ya malus ni zaidi ya hekta 600, matunda ya malus yanayozalishwa huko yanachukua zaidi ya 60% ya jumla ya uzalishaji wa matunda hayo nchini China. Kati ya yake, matunda ya malus yenye pembe nane ni aina maalumu, ikichukua zaidi ya 80% ya jumla ya uzalishaji wa matunda ya malus ya aina hiyo nchini China. Kila mwaka maua yanapochanua, kote sehemu hiyo ni maua ya malus. Mti mmoja mkubwa unaweza kuzaa matunda ya malus karibu kilo 1,000, katika majira ya mpukutiko majani, miti yenye matunda mengi ya malus vilevile ni kivutio kikubwa."

    Maua malus yenye pembe nane husifiwa sana na watu tangu zamani, hivyo miti hiyo mara kwa mara ilipandwa kwenye bustani za kifalme. Miti ya malus huchanua maua mwishoni mwa mwezi Aprili, na inazaa matunda katikati ya mwezi Mei baada ya maua kupukutika. Maua malus yanapoanza kuchanua yanakuwa na rangi ya kupendeza ya waridi nyepesi. Mtu anapoingia kwenye shamba la malus, anaweza kusikia harufu nzuri ya kunukia, mtalii You Jia alisema,

    "Ninakula matunda ya malus, lakini sijawahi kuona maua yake, leo ni mara ya kwanza kuona maua ya malus, tena ni kwenye eneo kubwa, maua yananivutia na kuniburudisha sana. Nimepiga picha nyingi, nitawaonesha jamaa zangu."


    1 2 3
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako