Kila mwaka wakati majira ya joto yanapoingia baada ya majira ya Spring, maua ya malus yanaanza kuchanua, vipande vya maua vinafunguka taratibu, vikaonekana kuwa na chavua za rangi ya waridi, ambazo zinabadilika polepole kuwa waridi nyepesi na yenye rangi nyeupe, huo ni wakati ambao maua malus yanapendeza zaidi. Katika siku chache za mwisho kabla ya maua malus kupukutika, maua hayo yanabadilika kuwa na rangi nyeupe na kidogo kuwa na rangi ya kijani, chavua zinaonekana kuwa na rangi ya manjano.
Mji mdogo wa Xiaonanxinbao ulipanda miti ya malus toka zamani sana, miti ya malus inaweza kuota kwa miaka 50 hadi 60 hivi, baadhi ya miti inaweza kuota kwa kiasi cha miaka 100, na kuwa na unene wa mita 1 hivi. Hebu fikiria maua ya malus yanayochanua kwenye eneo la kilomita za mraba 200, yakiongezwa pamoja na maua ya matufaha, mapea, allspice, Shaguo, Bingo, mizabibu, mitende na maua mengine ya milimani na ya porini, huko kabisa kunakuwa kama ni bahari ya maua. Kwa hiyo kila mwaka maua yanapochanua, shamba la malus huvutia idadi kubwa ya watalii. Mtalii kutoka Beijing Bw. Wamg Jinsong alisema,
"Nilifurahi zaidi nilipokuwa kwenye mlima mdogo, niliona shamba la malus pamoja na maji ya bwawa la Guanting, nilifurahi kweli kweli. Sura ya ardhi ya hapa inapendeza, na rasilimali za hapo ni nyingi, sehemu hii ina jangwa na vilima, kama tukitazama mbali tunaweza kuona milima mikubwa."
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |