• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kuangalia maua malus huko Huailai, mkoani Hebei

    (GMT+08:00) 2009-06-01 16:37:52

    Wakati wa adhuhuri, mwangaza wa jua ni wa kupendeza zaidi, baada ya kutembelea shamba la malus, watu wanasikia uchovu, wanatandika nguo au kuweka karatasi chini ya miti, wengine wanakaa kwenye meza za chakula za wakulima, na kuanza kupika chakuka wao wenyewe. Baadhi ya wageni wanakula chakula na vinywaji walivyobeba wenyewe, na wengine wananunua chakula kwenye vibanda vya wakulima wenyeji vinavyouza vyakula vya aina mbalimbali vikiwa ni pamoja na samaki, kamba wakubwa na chaza wa Ziwa Guanting, mboga pori za aina mbalimbali na uji wa uwele, maandazi yaliyokaangwa kwa unga wa ngano ulioivishwa kwa mvuke, matufaha, mapea, zabibu na malus yenye pembe nane, ilimradi ni chakula maalumu cha huko. Mbali ya kula chakula cha wakulima, wanakaa kwenye nyumba za wakulima, kufanya kazi za kilimo, kujiburudisha kwa vivutio vya kijijini, na kuishi maisha ya wakulima. Mtalii You Jia alirudi kwenye nyumba ya mkulima, akiwa na furaha baada ya kutoka matembezini, alifurahia chakula na maisha ya wakulima, akisema.

    "tulizoea kuishi katika mji mkubwa, leo tumefika mji mdogo wa kale wa Xiaonanxinbao kushuhudia maisha na mazingira ya kijijini, tumeshuhudia hali halisi ya nyumbani kwa wakulima, kwa uhakika tunajisikia tuko katika mazingira ya asili."

    Baada ya kutembelea shamba na kuangalia maua malus, watalii wanaweza kujiburudisha kwenye mashua katika Ziwa Guanting na kukamata samaki, kamba na chaza, vilevile wanaweza kutembea kwa boti kwenye ziwa hilo, na kufanya mashindano ya mbio ya mitumbwi mirefu yenye kichwa cha dragon; wanaweza pia kucheza mchezo wa kuteleza chini kutoka juu kwenye mwinuko wa mchanga, kupanda farasi na ngamia, kuendesha gari linaloweza kutembea jangwani, na kushuhudia vivutio vya jangwa …… yote hayo ni vitu visivyoweza kupatikana kwa wakazi wa mijini. Wanaweza kupumzika vizuri kwenye sehemu yenye mandhari nzuri, milima, mito ya kupendeza na yenye harufu nzuri ya maua kutoka katika maisha ya mjini yenye kazi nyingi na za haraka, msongamano wa watu na magari, tena kuna vitu vingi visivyochafua mazingira. Furaha na burudani, ambayo watu hawawezi kuvipata katika sehemu nyingine isipokuwa katika sehemu hii.


    1 2 3
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako