• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Zhangjiajie yajitambulisha duniani

    (GMT+08:00) 2009-06-08 16:47:33

    Sehemu yenye mandhari nzuri ya Zhangjiajie ni pamoja na bustani ya misitu ya taifa ya Zhangjiajie, hifadhi ya maumbile ya bonde la Suoxi na hifadhi ya maumbile ya Mlima Tianzi. Hivi sasa sehemu hiyo inajulikana sana duniani kwa kuwa na milima mikubwa, misitu minene na yenye vivutio vingi.

    Mliyosikia ni sauti ya sherehe ya ufunguzi wa "tamasha la utalii la kimataifa la Hunan, China mwaka 2008", sherehe hiyo ilifanyika hivi karibuni kwenye uwanja wa Laomowan wa bustani ya misitu ya Zhangjiajie. Watalii walioshiriki kwenye sherehe hiyo walivaa nguo zenye umaalumu wa kabila la huko na kuketi chini kwenye uwanja wa Laomowan wakiangalia mandhari ya kimaumbile ya kuvutia na maonesho murua ya michezo ya jadi ya huko, ambao walifurahi sana.

    "Anga ya buluu ni kama pazia, na ardhi ni kama jukwaa la michezo, vitu vyote ni vya kupendeza, hii inaonesha utamaduni wa kikabila wa mkoa wa Hunan, ambao ni mkubwa na kuonesha hali ya kuungana kwa binadamu na mazingira ya asili."

    Huu ndio mvuto wa Zhangjiajie, milima na mito ya kupendeza, sura ya ardhi ya huko ni ya kipekee, ambapo mawe ya milimani ni ya mabonde makubwa ya mchanga wa quartz, 98% ya sehemu hiyo ni misitu inayojaa hewa yenye oxygen hasi laki moja kwa eneo la kila sentimita za ujazo, vitu hivyo vinafanya watalii waliofika huko waipende sana sehemu hiyo.


    1 2 3
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako