• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Zhangjiajie yajitambulisha duniani

    (GMT+08:00) 2009-06-08 16:47:33

    Mwaka 2001 Zhangjiajie ilianza kutekeleza "kanuni za hifadhi ya urithi wa kimaumbile wa dunia wa Wulingyuan wa mkoani Hunan. Hii ni sheria ya kwanza ya ngazi ya kimkoa ya kulinda mali ya urithi wa maumbile ya dunia; mwaka 2004 idara husika ya serikali ya huko ikishirikiana na kampuni ya Microsoft iliweka "Dirisha la Zhangjiajie" linalotangaza moja kwa moja kwenye mtandao wa internet, ambalo ni la kwanza duniani, hivi sasa video kuhusu mandhari ya Zhangjiajie inaoneshwa kwa saa 24 kila siku, ili kuwawezesha watalii kutazama mandhari ya Zhangjiajie, kwa upande mwingine inaonesha nia ya sehemu hiyo yenye mandhari nzuri ya kutaka kusimamiwa na umma.

    Tarehe 11 mwezi Septemba mwaka huu, hoteli ya kwanza utalii ya nyota 5 ya kimataifa ya Wulingyuan ilizinduliwa huko Zhangjiajie, ikionesha kuwa huduma ya hoteli za utalii za Zhangjiajie inaingia kwenye ngazi ya nyota tano. Kuhusu suala hilo, mwenyekiti wa kikundi cha washauri cha jumuiya ya utalii ya Thailand Bw. Li Chaowen alisema,

    "Nilifika hapa miaka 6 au 7 iliyopita, ninaona kuna mabadiliko makubwa, kazi za hoteli ni nzuri sana, zana mbalimbali pia ni nzuri, milima na mito ni mizuri kama zamani."

    Baada ya kupotea kwa bahari, mabadiliko mengi yalitokea kwenye ardhi ya sehemu ya juu ya dunia. Katika muda wa zaidi ya miaka milioni 380 iliyopita, milima 3,000 na mito 800 ilitokea, lakini katika muda mfupi wa miongo kadhaa, jina la Zhangjiajie limejulikana kote duniani. Hivi sasa Zhangjiajie inapiga hatua haraka kuelekea kuwa mji wa utalii wa kimataifa, na kufikia kipindi cha pili cha maendeleo makubwa. Naibu mkurugenzi wa idara ya utalii ya taifa Bw. Zhang Xiqin alisema,

    "Ni kweli kwamba sekta ya utalii ya Zhangjiajie ilikwenda sambamba na hatua za maendeleo ya sekta ya utalii ya China, Zhangjiajie ni mfano mzuri wa maendeleo ya sekta ya utalii ya China, ni alama na ni picha ya kweli".


    1 2 3
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako