Katika majira ya mchipuko ya mwaka 1979, mwandishi wa habari wa shirika la habari la China Xinhua Bw. Yang Fei aliyekuwa na umri wa miaka 32 alikuwa mtu wa kwanza kupiga picha kwenye sehemu ya Zhangjiajie, ambazo baadhi yake zilichapwa kwenye jarida la "Jiografia" la Marekani. Hizo zilikuwa picha za awali kabisa zinazowajulisha watu kuhusu Zhangjiajie. Kwa wakazi wa Zhangjiajie, mtu aliyetoa mchango mkubwa zaidi ni bingwa mchoraji wa michoro ya kichina Bw. Wu Guanzhong. Naibu meya wa Zhangjiajie Bw. Xiao Lingzhi alisema,
"Wu Guanzhong alikwenda huko kuchora michoro, siku moja aligundua sehemu moja ya kupendeza, ambayo watu walikuwa hawaifahamu, hivyo akaandika makala moja isemayo "Watu hawamfahamu mwanamwali aliyewekwa ndani", vilevile michoro ilitolewa, hivyo dunia ikaijua sehemu hiyo."
Makala hiyo ya Gu Guanzhong iliishangaza sekta ya utalii, baada ya hapo mpiga picha bingwa Chen Fuli alituma picha alizopiga ziitwazo "Picha za mwewe wa mlimani" kushiriki kwenye maonesho ya jumuiya ya wapiga picha ya kifalme ya Uingereza, ambazo zilipewa tuzo ya dhahabu, watu wa Ulaya kwa mara ya kwanza walilifahamu jina la zhangjiajie.
Bustani ya kwanza ya misitu ya taifa ya China ilijengwa huko Zhangjiajie mwaka 1982; mwaka 1992 Wulingyuan ya Zhangjiajie iliorodheshwa kwenye orodha ya mkupuo wa kwanza wa urithi wa kimaumbile wa dunia, mwaka 1994 sehemu ya Zhangjiajie yenye mandhari nzuri ilithibitishwa kuwa mji wa ngazi ya mkoa na kuwa mfano wa shughuli za utalii nchini China. Hivi sasa Zhangjiajie imekuwa mahali panapopendwa na watalii wa nchini na wa nchi za nje.
Mandhari ya Zhangjiajie ni pamoja na vivutio vya milima, misitu, mapango, maziwa na maporomoko ya maji. Katika kando mbili za mto mdogo wa Jinbian kwenye sehemu yenye mandhari nzuri ya Wulingyuan, kuna miti mikubwa sana iliyoota kwa miaka mingi, ambayo majani yake mengi yanazuia mwanga wa jua. Lakini zaidi ya nusu karne iliyopita, watu hawakuufahmu mto Jinbian. Katika sehemu ya Wulingyuan yenye rasilimali kubwa ya utalii, mkuu wa wilaya Bw. Chen Hongri alisema, kama isingekuwa na shughuli za utalii, sehemu hiyo ingekuwa na sura yake ya zamani. Alisema,
"Hapo zamani nyumba za wakazi wa sehemu hiyo zilikuwa ndogo na ziliezekwa kwa manyasi, watoto hawakupata nafasi ya kwenda shule. Baada ya kuendelezwa kwa shughuli za utalii, wakazi wa huko wamekuwa na nyumba zenye ghorofa. Hivi sasa karibu theluthi moja ya wakazi wa Wuling wanashiriki moja kwa moja kwenye shughuli za huduma za utalii, na 85% ya pato la serikali ya huko linatokana na shughuli zinazohusika na utalii."
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |