• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tambi za Hainan, chakula maarufu kwenye mtaa wa zamani wa Haikou

    (GMT+08:00) 2009-07-20 15:18:52

    Mandhari ya kuvutia ya Hainan

    Mkoa wa Hainan ulioko kwenye bahari ya kusini ya China ni mahali maarufu sana kwa mapumziko. Licha ya kuwepo kwa mandhari nzuri ya bahari na anga ya buluu, fukwe na misitu ya minazi ya kupendeza, kuna aina mbalimbali za vyakula vyepesi maalumu. Na sasa tunawaelezea kuhusu tambi za Hainan, ambazo ni chakula maarufu zaidi mkoani Hainan.

    Mji wa Haikou kila siku unaanza kuwa na pilikapilika kuanzia saa 12 asubuhi, ambapo mkahawa wa tambi za Hainan wa shangazi Pan unapata wateja wengi. Mwenye mkahawa shangazi Pan Xuanmei na mke wa mwanawe Luo Haizhen wanawaandalia wateja chakula cha tambi nyeupe za unga wa mchele zilizotiwa karanga, ufuta, vimeo vya maharage, vipande vyembamba vya nyama ya ng'ombe, giligilani na mchuzi mzito, chakula hicho kina rangi mbalimbali za kupendeza na viungo vya kunukia, na kinaongeza shauku ya watu ya kula.

    Baada ya saa 3 asubuhi, wateja wanaanza kupungua, ambapo shangazi Pan anaweza kupata nafasi ya kupumzika kidogo. Shangazi Pan si hodari wa kuzungumza na watu, mkwe wake Luo Haizhen alisema, mkahawa wao ulianzishwa mwaka 1987, na sasa imepita zaidi ya miaka 20 tangu uanzishwe. Alisema:

    "Kuuza tambi za Hainan ni shughuli zetu za jadi, tulianza shughuli hizi toka enzi ya babu yetu."

    Bi. Luo Haizhen alisema, wateja wengi wanapenda tambi zao, kila siku hawakosi kwenda kula huko. Bw Peng ni mmoja kati ya watu hao. Alisema

    "Vitu vinavyotumiwa na wapishi wa mkahawa huo ni vizuri zaidi kuliko vya mikahawa mingine, nafika hapa mara kadhaa kwa wiki, na napenda kula tambi hapa kila ninapopata nafasi."

    Bi. Luo Haizhen alisema kila siku yeye na mama mkwe wake wanaamka saa 11 alfajiri, na kuandaa viungo zaidi ya aina 10 pamoja na mchuzi wa kombe wa baharini. Kazi za kutengeneza tambi za Hainan si rahisi, kwa hiyo tambi zinazotumiwa katika mkahawa wao zinanunuliwa kutoka kwa wapishi maalumu wa tambi. Wanafungua mkahawa saa 12 asubuhi, na shughuli zinaendelea hadi saa 8 mchana. Kila siku wananunua zaidi ya kilo 100 za tambi, na tambi zote wanazopika zinanunuliwa siku hiyo na wateja. Bi Luo Haizhen alisema:

    "Chakula cha mkahawa wetu ni safi, hakuna chakula kinachosalia na kuuzwa siku ya pili, ladha ya chakula chetu ni nzuri, kwa sababu vitu tunavyotumia vyote ni bora, supu inayotiwa katika tambi vilevile inapikwa kila siku kwa zao la kombe zaidi ya kilo 20."


    1 2 3
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako