• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tambi za Hainan, chakula maarufu kwenye mtaa wa zamani wa Haikou

    (GMT+08:00) 2009-07-20 15:18:52

    Tambi za hainan

    Tambi za Hainan zinaliwa zikiwa baridi. Kwanza tambi zilizokwisha chemshwa zinatiwa katika bakuli, kisha vinatiwa viungo na vitoweo, na mwisho unamiminwa mchuzi uliopikwa kwa vipande vyembamba vya figili, auricularia, vichipukizi vya mianzi na day lily, hiki ndiyo chakula cha tambi cha kuvutia watu. Kwa kuwa tambi zilizochemshwa zinatiwa katika maji baridi, hivyo tambi zinakuwa baridi, lakini baada ya mchuzi kupashwa, chakula hicho cha tambi kinakuwa sio baridi wala sio moto. Wateja baada ya kuandaliwa chakula cha tambi, kwanza wanachanganya vizuri tambi, viungo na mchuzi kwa vijiti vya kulia, kama zikitiwa pilipili kidogo tambi zitakuwa nzuri zaidi.

    Endapo mtu atakula haraka na kuzimaliza tambi hizo zote, itakuwa jambo la kusikitisha, kwani ulaji wa tambi za Hainan ni tofauti na tambi za sehemu nyingine, yaani tambi zinapobaki kidogo katika bakuli, supu ya kombe inatiwa katika bakuli, baada ya kunywa supu hiyo mtu anajisikia vizuri zaidi. Naibu kiongozi wa jumba la sanaa la Haikou, ambaye ni mtaalamu wa mila ya jadi Bw. Qiu Tianwei alisema, amefanya utafiti sana kuhusu chakula cha tambi cha Hainan. Alisema:

    "Tambi za Hainan zina harufu na ladha nzuri, mtu anapokula anaona ladha yake ni tofauti na tambi zilizotengenezwa kwa unga wa ngano. Kwa kuwa Haikou iko karibu na bahari, kwa hiyo supu iliyopikwa kwa kombe na chaza wa baharini ina ladha nzuri, mtu akila bakuli moja la tambi, halafu anakunywa supu ya chakula cha baharini anajisikia vizuri zaidi, hii pia inaambatana na umaalumu wa Hainan."

    Tambi za Hainan zimekuwa na historia ya zaidi ya miaka 500, tena kuna hadithi moja husika ya kusisimua. Inasemekana kuwa katika kipindi cha mwisho cha enzi ya Ming, kulikuwa na fundi mmoja aliyeitwa Chen kwenye sehemu ya kusini ya Fujian, fundi huyo na mama yake walihamia kwenye mji wa zamani wa Chengmai wa Hainan, mama yake alikuwa dhaifu kwa kuugua mara kwa mara, tena alikuwa hana hamu ya kula. Fundi huyo kijana alipoona mchele mtamu na maji safi ya huko akapata wazo la kutengeneza tambi kwa unga wa mchele, baada ya kula tambi za aina hiyo, mama yake alipata hamu ya kula, na afya yake ikaanza kuwa nzuri polepole. Upendo wa fundi Chen ukasifiwa na watu, na kuanza kuenezwa kama hadithi. Hapo baadaye alifungua sehemu ya kusaga mchele na kutengeneza tambi, kutokana na ufundi alioutumia na mchele wake kuwa mzuri, tambi zilizotengenezwa naye zilikuwa nyeupe na laini sana, watu walizipenda sana, hivyo watu wengi walimfuata ili kujifunza ufundi wake. Baadaye tambi za aina hiyo zilizovumbuliwa naye zikaitwa "tambi za Hainan" na kuenea katika kisiwa kizima.

    Hadi sasa watu wanazipenda tambi za aina hiyo. Tambi zinazouzwa kwenye mikahawa ya mtaa wa Laojie wa Haikou ni za asili na zenye ladha nzuri zaidi, ingawa mikahawa hii ni midogo na siyo ya kifahari, lakini tambi zinazouzwa huko ni nzuri na za bei rahisi zaidi.


    1 2 3
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako