wakazi wa Hainan wakiwa wanakula tambi za Hainan
Hapo zamani tambi za Hainan zilitumiwa kama chakula chepesi na haraka, lakini sasa zimekuwa ni chakula kinachopendwa sana na watu. Sasa wakazi wa Haikou wanazitumia katika siku za kawaida na hata katika sikukuu. Wakazi wa Haikou wanapowakaribisha watu, hupenda kusema, "hebu twende nyumbani tukale tambi!". Tambi za Hainan zinapendwa sana na wakazi wa huko na zinachukuliwa kama ni kitu kisichoweza kukosekana katika maisha yao, hasa kwa wenyeji wa huko waliohamia sehemu nyingine. Kijana Chen ni mwanafunzi aliyesoma katika sehemu ya nje kwa miaka 4, huwa ana uchungu mwingi kuhusu kuzikosa tambi za Hainan. Alisema:
"Nikiwa sehemu ya nje, niliwahi kula tambi za Dandan, tambi za unga wa mchele za Guilin, Guangxi, tambi za He za Guangzhou na tambi zilizopikwa pamoja na kababu za nyama ya ng'ombe, lakini ninaona tambi zetu za Hainan ni nzuri zaidi."
Ni bora ushuhudie mwenyewe kuliko kusikia. Endapo utapata nafasi ya kwenda Hainan, licha ya kuangalia mandhari nzuri ya huko, usisahamu kutembelea mitaa au vichochoro vya Haikou, vilevile usisahamu kwenda kuonja tambi za Hainan zilizotengenezwa na wenyeji wa huko, tena zinauzwa kwa bei rahisi, Yuan 3 au 4 tu.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |