• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Nyimbo za kabila la Wahani mkoani Yunnan

    (GMT+08:00) 2009-08-06 16:58:49

    Mkoa wa Yunnan ulioko kusini magharibi mwa China una makabila 26 madogo madogo, ambapo ni mkoa wenye makabila madogo madogo mengi zaidi nchini China. Kabila la Wahani ni moja kati ya makabila hayo. Lugha ya kabila hilo haina maandishi, hivyo historia, utamaduni na mambo mengine ya maisha ya kabila hilo yanarithiwa kwa midomo, hata kwa njia ya nyimbo kizazi baada ya kizazi. Wilaya inayojiendesha ya kabila la Wahani ya Mojiang mkoani Yunnan ni wilaya pekee ya inayojiendesha ya kabila hilo nchini China, na nyimbo za kabila hilo zilizoenea katika wilaya hiyo ni maarufu sana.

    Watu wa kabila la Wahani wanapenda kueleza hisia zao kwa kuimba nyimbo wakati wanapofanya kazi za kilimo. Licha ya hayo, nyimbo wanazoimba pia zinahusu mambo mbalimbali ya maisha yao, yakiwemo desturi ya kuwatendea watu, historia, utamaduni, sanaa, elimu ya unajimu, jiografia na upandaji wa mimea. Naibu mkurugenzi wa idara ya utamaduni na michezo ya wilaya ya Mojiang Bw. Li Weizhong alisema,

    "Uhusiano kati ya muziki wa kabila la Wahani na lugha ya kabila hilo unafanana na ule wa lugha ya kichina ya kale na ya kisasa. Maneno kwenye nyimbo za kabila hilo yote ni ya kale."

    mliosikia ni wimbo uitwao "Jilong" ulioimbwa na mwimbaji mkulima wa kabila la Wahani Bi Wang Meifeng. Katika wimbo huo anasema ndege wanalia, kwani wakati wa kupanda mbegu wadia. Mimea ya mpunga ya rangi ya kijani, yaonekana kama inacheka cheka. Bw. Li Weizhong alisema watu wa kabila la Wahani wanaimba nyimbo tofauti katika sehemu tofauti, kwa mfano, hawawezi kuimba nyimbo zinazoimbwa milimani nyumbani kwao, kwa kuwa nyimbo hizo ni za kueleza mapenzi kati ya vijana, pia hazifai kuimbwa nyumbani kwani kuna wazee na watoto.


    1 2 3
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako