• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Nyimbo za kabila la Wahani mkoani Yunnan

    (GMT+08:00) 2009-08-06 16:58:49

    Hivi sasa serikali katika ngazi ya wilaya ya Mojiang wakati inapoendeleza uchumi ili kuboresha maisha ya watu, pia inatilia maanani sana kulinda utamaduni wa kabila la Wahani, na inafanya juhudi kubwa za kulinda na kurithisha nyimbo za kabila hilo. Kwa hatua ya mwanzo, nyimbo hizo zimeingizwa kwenye madarasa ya shule za msingi na sekondari, elimu ya nyimbo hizo zinafundishwa kwa wanafunzi watoto, pia wanafundishwa kuimba nyimbo hizo. Aidha, wilaya hiyo pia inavihamasisha vijiji vyake mbalimbali vianzishe vikundi vya maonesho ya nyimbo na ngoma za kikabila, na kutengeneza VCD za nyimbo hizo, ili kuongeza athari ya sanaa hiyo ya kabila la Wahani, mbali na hayo wilaya hiyo inaandaa mashindano ya nyimbo na ngoma kila mwaka au kila baada ya mwaka mmoja. Bw. Li Weizhong alisema,

    "Zikiwa ni za utamaduni usioonekana, nyimbo za kabila la Wahani ni mali yenye thamani kubwa iliyorithiwa na mababu wa kabila hilo. Sasa tunarithi na kuendeleza nyimbo hizo kwa njia inayofaa, ili kuzifanya ziwe za kung'aa zaidi."


    1 2 3
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako