• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Nyimbo za kabila la Wahani mkoani Yunnan

    (GMT+08:00) 2009-08-06 16:58:49

    Bw. Li Weizhong alijulisha kuwa, nyimbo za kabila la Wahani zina lahani tofauti, na lahani hizo zinatokana na mgawanyiko wa tangu zama za kale. Alisema kabila la Wahani lina matawi tisa ya Kado, Biyo, Hauni, Baihon, Lami, Chedi, Amuu, Kabi na Simoluo, na lahani za nyimbo za wahani kutoka matawi hayo pia ni tofauti sana.

    Mliosikia ni wimbo ulioimbwa na mwimbaji mkulima wa tawi la Kado Bw. Dao Hongcheng. Bw. Li Weizhong alisema lahani ya nyimbo za watu wa matawi ya Kado na Biyo ni za chini na za kusikitisha, lakini nyimbo za matawi ya Hauni na Baihon ni za furaha.

    Mliosikia ni wimbo ulioimbwa na Bi Wang Meifeng kutoka tawi la Hauni la kabila la Wahani, sasa tusikilize wimbo unaoimbwa na watoto wawili kutoka tawi la Baihon.

    Baadhi ya nyimbo za kabila la Wahani zinaimbwa na wanawake tu, kwa mfano nyimbo za kuwabembeleza watoto walale. Sasa tusikilize wimbo huo unaoimbwa na Bi Ren Liqing kutoka tawi la Simoluo la kabila la Wahani.

    Nyimbo zinazoimbwa zaidi na watu wa kabila la Wahani ni nyimbo za mapenzi. Wavulana na wasichana wanaelezeana mapenzi yao kwa kuimba nyimbo katika mashamba au misitu. Sasa tusikilize wimbo wa mapenzi wa kabila la wahani.


    1 2 3
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako