• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kutembelea Luoyang wakati maua yanapochanua

    (GMT+08:00) 2009-08-10 15:59:32

    Toka zamani za kale, maua ya peony yanapendwa sana na watu wa China kutokana na uzuri wake wa hali ya juu. Mji wa Luoyang wa mkoa wa Henan, sehemu ya kati ya China ni mji uliofanywa kuwa mji mkuu katika enzi nyingi kwenye historia ya China. Mji wa Luoyang unajulikana sana kutokana na historia na utamaduni wake, vilevile kwa maua ya peony. Hali ya hewa ya Luoyang si ya joto wala baridi sana, ardhi yake ina rutuba nyingi, zaidi ya hayo kutokana na ufundi wa mabingwa wa upandaji wa maua, maua ya peony yamesifiwa kuwa ni mazuri kuliko maua mengine yote duniani.

    Sasa maua ya peony yamekuwa na historia ya zaidi ya miaka 1,600 tangu yapandwe kutoka katika hali yake ya zamani ya kimwitu. Tokea enzi ya Tang, maua ya peony yanachukuliwa kama maua yanayotia fora nchini China. Endapo watu wanapiga kura kuchagua ua la kitaifa, bila shaka maua ya peony yatachaguliwa na watu. Ingawa enzi nyingi zilibadilika, lakini hadhi ya peony ambayo ni kama mfalme wa maua inaendelea hadi sasa.

    Maua ya peony yalipandwa na wakazi wa Luoyang toka zamani, na jina lake lilianza kuvuma nchini kabla ya zaidi ya miaka 1,000 iliyopita. Mji wa Luoyang hufanya "tamasha la maua ya peony" kila mwaka tokea mwaka 1983, ambapo idadi kubwa ya watalii na wafanyabiashara huenda huko kwa matembezi.

    Meya wa Luoyang Bw. Guo Hongchang alisema,

    "Hivi sasa, tamasha la maua ya Luoyang limekuwa kama shughuli za siku kuu zikiwa na matembezi ya kuangalia maua kwenye bustani, kufanya matambiko kwenye makaburi ya wazee, maingiliano ya kiuchumi burudani na utalii. Mwaka 2007 tamasha hilo lilithibitishwa kuwa moja ya siku za aina kumi za maua nchini China, na kuorodheshwa katika orodha kuwa mabaki ya kiutamaduni yasiyo ya vitu ya ngazi ya taifa mwaka 2008.


    1 2 3
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako