Kila mwaka inapofika mwezi Aprili na May, maua ya peony yanachanua vizuri zaidi na kuvutia watalii wengi.
Mtalii kutoka mji wa Zhengzhou Bi. Chen Liyan alisema,
"Naona maua ya peony yanafaa kuwa ua la kitaifa, najisikia furaha sana wakati ninapoyaona, tena ninahisi majira ya Spring yanawadia."
Hivi sasa, mahali penye maua mengi zaidi ya peony mjini Luoyang ni bustani ya maua ya taifa ya China na bustani ya mji wa mfalme. Maua ya peony yanapendeza zaidi katika mwanga wa jua katika majira ya Spring. Mtalii kutoka New York, Marekani anaeleza furaha yake kuhusu maua ya peony kwa lugha ya Kichina aliyojifunza, alisema:
"Peony ya Luoyang inatia fora duniani!"
Maua ya peony yanachanua kwa muda mrefu zaidi kutoka mwishoni mwa mwezi Machi hadi mwanzoni mwa mwezi Mei. Wakati maua ya peony yaliyopandwa katika sehemu za mzunguko wa mji wa Luoyang yanapokaribia kunyauka, maua ya peony katika bustani zilizoko kwenye eneo la mlima la kusini mwa Luoyang bado yanachanua vizuri.
Kwa sababu, sehemu ya Luoyang inarasilimali nyingi za maua ya peony, ambayo ni moja ya sehemu zenye peony pori nchini China. Aina nyingi za maua ya peony zimeoteshwa kutokana na maua ya peony ya asili ya Luoyang. Maua hayo mwitu ya peony yanachanua kwa muda mrefu zaidi, maua yenyewe ni mazuri na ya kupendeza zaidi.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |