• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kutembelea Luoyang wakati maua yanapochanua

    (GMT+08:00) 2009-08-10 15:59:32

    Naibu mkurugenzi wa idara ya usimamizi wa mlima Baiyun ya wilaya ya Song, mkoani Henan Bw. Wang Guangyi alisema,

    "Katika bustani ya peony ya Gaoshan ya sehemu ya mandhari ya mlima Baiyun kuna maua mwitu ya peony ya mlimani, ambayo yanapatikana kwa nadra sana hivi sasa, maua hayo ni tofauti kabisa na maua ya peony yanayooteshwa na watu. Maua hayo yanachanua vizuri zaidi baada ya tarehe 10 mwezi Mei, nyakati za kuchanua zinaendelea hadi tarehe 10 hivi mwezi Juni.

    Tamasha la maua ya peony la mwaka huu liliambatana na maonesho mengi ya michezo ya sanaa. Toka tarehe 1 mwezi Aprili maonesho ya nyimbo na ngoma yalifanyika katika bustani ya maua ya taifa ya China, ambapo watalii licha ya kuweza kuona maonesho ya michezo ya sanaa, wanaweza pia kuuhisi utamaduni wa peony.

    Kwenye uwanja wa mbele wa sehemu ya mandhari ya Guanlin, mjini Luoyang, ilioneshwa michezo ya opra kwenye jukwaa, watalii kutoka sehemu mbalimbali walikuwa wakisikiliza kwa shauku kubwa. Mfanyakazi wa sehemu hiyo alisema, maonesho ya michezo ya utamaduni yanavutia sana watalii hata watalii kutoka nchi za nje, hivyo wanakaa kwa siku nyingi zaidi kwenye sehemu hiyo yenye mandhari ya kuvutia.

    Baada ya kuona maonesho ya michezo, mtalii kutoka mji wa Zhunyi alisema,

    "Licha ya kuona maua, tumeona maoensho ya sarakasi, nyimbo zikiimbwa na ngoma, naona ni nzuri sana, nilifika katika sehemu nyingi, lakini sikuona kama ya hapa, nitawafahamisha marafiki zangu na kuwataka wafike huko kuangalia."


    1 2 3
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako