• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matembezi ya furaha kwenye Mlima Chishan

    (GMT+08:00) 2009-08-10 16:03:17

    Kisiwa cha Shidao kilichoko upande wa mashariki kabisa ya penisula ya Shandong iliyoko sehemu ya mashariki ya China ni mahali penye mandhari nzuri ya kuvutia, hapa panaitwa na watu kuwa ni "Hong Kong ndogo ya kaskazini".

    Sehemu ya mandhari ya Mlima Chishan ina kilomita za mraba 12.8, sehemu hii iko karibu na bahari ya Huang, na inasifiwa na watu kuwa ni baa ya oksijin(oxygen) kutokana na kuwa na msitu wenye hekta 1,000. Kuna njia nyingi ndogo zinazoelekea sehemu ya ndani ya msitu ambayo ina mazingira yasiyo na makelele, vijito, milio ya ndege na maua ya kunukia. Mbali na hayo, watu wanaweza kuona mahekalu, utamaduni, mila za jadi, mabaki ya kiutamaduni ya Korea ya kusini na Japan.

    Muziki wa dini ya kibudha unatuvutia hadi kwenye eneo la Buddha ambalo ni kama Peponi(Paradise) lililoko sehemu ya kati ya eneo la mandhari ya Mlima Chishan. Eneo hilo lina sanamu moja ya Budha Guanyin iliyotengenezwa kwa shaba nyeusi zaidi ya tani 200 pamoja na sanamu nyingine ndogo, chemchemi, maporomoko ya maji, muziki na moto.

    Watoto wawili mmoja wa kike na mwingine wa kiume, ambao ni watumishi wa Buddha Guanyin wakiambatana na sauti ya muziki wa dini ya kibudha, walitoka taratibu wakachukua trei na kudaka matone ya maji yaliyotoka kwenye chupa aliyoishika mkononi Guanyin.

    Hapo watawa wanaanza kusoma msahafu, sanamu ya Guanyin nayo inaanza kugeuka taratibu kama vile inaangalia sehemu mbalimbali za Mlima Chishan. Kwa kufuata mdundo wa muziki wa dini, maji yanarushwa juu angani kwa zaidi ya mita 30, watendaji wanne wa Jingang walioko chini ya tandiko analoketi Buddha Guanyin, wanatoa moto midomoni, budhaa wengine walioko pembezoni nao wanaonekana kama wakicheza ngoma, vinyago 9 vya dragon vya rangi ya dhahabu vilivyoko katika bwawa la chemchemi vinatoa maji midomoni. Chini ya mwanga wa jua, sanamu kubwa ya Guanyin inazungukwa na maji, ambapo upinde wenye rangi saba unaonekana kama mwanga wa budhaa.


    1 2 3
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako