• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matembezi ya furaha kwenye Mlima Chishan

    (GMT+08:00) 2009-08-10 16:03:17

    Mbali na hekalu la kibudha na masimulizi kuhusu Japan na Korea ya kusini, liko jumba moja la makumbusho ya mila na utamaduni wa sehemu ya mashariki ya mkoa wa Shandong. Ndani ya jengo hilo kuna kumbi 3 zenye maeneo 6 ya maonesho, picha, sanamu na vitu vilivyoko huko vinaonesha mila, utamaduni na maisha ya watu wa huko.

    Mwongoza watalii Bw. Zhang Dan alisema,

    "Nyumba moja iliyoezekwa kwa nyasi za baharini imedumu kwa miaka 100 hivi, nyasi za baharini zinaota kwenye maji ya baharini yenye kina kati ya mita 5 na 10."

    Pamoja na maendeleo ya jamii, hivi sasa ni watu wachache sana katika sehemu ya mashariki ya mkoa wa Shandong, ambao bado wanaishi katika nyumba za aina hiyo. Ili kuwaonesha watalii utamaduni na maisha ya wakazi wa huko, nyumba moja iliyoezekwa kwa nyasi za baharini pamoja na vitu vilivyotengenezwa kwa nta vinavyohusiana na maisha ya watu vinaoneshwa katika jumba la makumbusho. Kati yake iko sanamu moja ya nta inaonesha msichana akipambwa kabla ya kuolewa siku hiyo. Zhang Dan alisema,

    "Msichana anatakiwa kuondolewa vinyweleo usoni kwa nyuzi zilizosokotwa; na chini ya kiti anachokaa limewekwa shoka moja, kwani sauti ya tamko la neno shoka ni sawa na tamko la neno la baraka, ikitumainiwa kuwa msichana huyu anayeolewa afikishe baraka nyumbani kwa mumewe."


    1 2 3
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako