• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matembezi ya furaha kwenye Mlima Chishan

    (GMT+08:00) 2009-08-10 16:03:17

    Kufuata njia ya ngazi za mawe inayozunguka-zunguka, tulifika kwa Budha Ming wa Mlima Chishan ambaye ni sanamu ya kwanza ya mungu wa bahari ya China. Kutokana na kuzungukwa na maji ya bahari kwa pande tatu, toka zamani za kale wakazi wa Kisiwa cha Shidao wanaishi kwa kutegemea kuvua samaki, na kuwa na mila pakee ya kuabudu mungu wa bahari. Sanamu hiyo ya mungu wa bahari ina kimo cha mita 58.8, na ilitengenezwa kwa shaba kwa ufundi wa kugonga kwa nyundo kubwa. Mungu huyu anachunguza baharini akiwa amekaa kwenye mlima na kulinda usalama wa watu waliokwenda baharini. Muongoza watalii Bi. Zhang Dan ni mkazi wa huko, alisema, jinsi mungu wa bahari anavyoweka mikono yake ina maana ambayo siyo ya kawaida, alisema:

    "Mungu Ming wa Mlima Chishan ni Rihuajun, mungu wa jua anayeabudiwa na watu wa China tokea enzi za kale, vilevile ni mungu muhimu aliyekuwa akiabudiwa na wafalme wa enzi mbalimbali, anaweka mkono wa kushoto kwenye goti lake, ikiwa na maana ya kufariji nyoyo za watu. Anaweka kiganja cha mkono wake wa kulia kuelekea chini, ikiwa na maana ya kutuliza mawimbi makali ya baharini, na kubariki wavuvi wapate samaki na kamba wengi."

    Inasemekana kuwa mungu Ming wa Mlima Chishan alimfariji Zhang Baogao wa Korea ya kusini aliyekuwa akisifiwa kuwa ni"mfalme wa baharini" kwa kufanikisha jitihada yake, aliondoa shida na hatari za baharini zilizomkumba mtawa mahiri Yuan Ren wa Japani, hivyo anaabudiwa na watu wa nchi tatu za China, Japan na Korea ya kusini.

    Inasemekana kuwa katika mwaka 790, Zhang Baogao alikwenda kujiunga na jeshi la enzi ya Tang, kutokana na ushujaa wake alipata mafanikio makubwa katika vita. Hapo baadaye alipofika kwenye Kisiwa cha Shidao alivutiwa na mazingira maalumu ya huko, akaanza kwenda na kurudi kati ya China, Japan na Korea ya kusini na kufanya biashara kwenye bahari. Kabla ya zaidi ya miaka 1,200 iliyopita, Zhang Baogao alianzisha njia mpya ya biashara ya baharini kutokana na akili yake. Ili kumkumbuka mtangulizi huyu wa biashara ya baharini na uundaji wa urafiki kati ya China na Korea ya kusini, wakazi wa kisiwa hiki waliweka jiwe kubwa lenye michoro ya sura yake kwenye ukumbi wa mungu Ming nyuma ya sanamu ya mungu Ming iliyoko kwenye Mlima Chishan. Mwongoza watalii, Bi. Zhang Dan alisema,

    "Mwaka 843, mtawa Yuan Ren wa Japan aliporejea nchini kutoka China katika enzi ya Tang alikumbwa na mawimbi makubwa baharini. Wanamaji waliokuwa katika jahazi hiyo walipiga magoti kuelekea upanda aliko mungu Ming kwenye Mlima Chishan na kuomba kusaidiwa na mungu Ming. Mungu Ming akatupa mshale wa amri angani kwa upinde, mara upepo na mawimbi ya baharini yakatulia, mtawa Yuan Ren alirudi kwa usalama. Baada ya mtawa kuiaga dunia, wanafunzi wake walitekeleza usia wake walijenga hekalu ya Mlima Chishan na kumuabudu mungu Ming."


    1 2 3
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako