• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kutalii kwenye maporomoko ya maji ya Detian yaliyoko kwenye mpaka kati ya China na Vietnam

    (GMT+08:00) 2009-10-12 16:55:47

    Maporomoko ya maji ya Detian yaliyoko kwenye wilaya ya Daxin, mkoa unaojiendesha wa kabila la Zhuang, wa Guangxi China ni maporomoko yanayochukua nafasi ya pili duniani na nafasi ya kwanza ya kuvuka mpaka barani Asia. Maporomoko ya Detian yako kwenye mpaka kati ya China na Vietnam. Sasa tanawaeleza kuhusu mandhari nzuri ya maporomoko ya Detian pamoja na urafiki kati ya China na Vietnam.

    Maji ya maporomoko ya Detian yanatoka mto Guichun, wilaya ya Jingxi, mkoani Guangxi, mto huu unaoingia Vietnam na kurudi katika mkoa Guangxi una maji katika majira yote ya mwaka. Maji ya mto huu yanapofika kwenye kijiji cha Detian, wilayani Daxin, yanaanguka moja kwa moja kutoka sehemu ya genge. Maji ya maporomoko ya maji hayo yanaungana na maji ya maporomoko ya maji ya Banyue ya Vietnam kwa upande wa kushoto, kwa jinsi inavyoonekana ni kama mapacha. Maporomoko ya Detian yako katika nchi mbili za China na Vietnam, maji yake yanaanguka kwa ngazi tatu, maporomoko hayo yana upana wa zaidi ya mita 100, unene zaidi ya mita 60 na kimo cha karibu mita 50.

    Mwongoza watalii kwenye sehemu ya maporomoko ya Detian alisema, mandhari ya maporomoko ya Detian ni tofauti katika majira manne ya mwaka. Mwanzoni mwa majira ya Spring, misufi iliyoko kwenye kando mbili za mto Guichun inachanua maua, maporomoko ya maji ya Detian yanaonekana kama ni mnyororo wa rangi nyeupe katika maua mengi ya rangi nyekundu. Yanapofika majira ya joto, sauti ya maporomoko inasikika kama ngurumo kubwa. Katika majira ya mpukutiko wa majani, mazao yaliyoko kwenye mashamba ya matuta yaliyoko kwenye mitelemiko ya milima yanabadilika kuwa na rangi ya dhahabu, maji ya maporomoko yanakuwa maangavu kabisa. Wakati baridi inapoingia huko, maji ya maporomoko yanapungua kwa udhahiri. Kwa jumla, toka mwezi Julai hadi mwezi Septemba kila mwaka ni kipindi chenye maji mengi, ambapo maporomoko ya maji huwa ni makubwa, na ni wakati mzuri zaidi wa kuangalia maporomoko ya maji. Mwongoza watalii alisema maporomoko ya Detian yana vivutio viwili.


    1 2 3
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako