Watu wanaotembelea sehemu ya maporomoko ya Detian, wanahisi kuwa milima na mito ya China na Vietnam inaungana, mtu akisimama kwenye kando ya mto Guichun anaweza kuona vibanda vilivyojengwa na watu wa Vietnam, tena anaweza kupata bidhaa za nchi hiyo kutoka kwa wafanyabishara hao. Bi Wu kutoka mji wa Wuhan alisema, hii ni mara yake ya kwanza kutembelea maporomoko ya Detian, anajionea mambo mawili, anasema.
"Maporomoko ni makubwa na yanapendeza; Maporomoko hayo mawili yananifurahisha sana kwa kuwa yameungana, naona milima inaungana, mito inaungana, nchi zinaungana, na urafiki unaunganishwa."
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |