• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bustani ya kijiolojia ya dinosaur ya Erlianhaote

    (GMT+08:00) 2009-10-19 16:59:10

    Mji wa Erlianhaote uko kwenye upande wa kaskazini wa mkoa unaojiendesha wa Mongolia ya ndani wa China, na ni forodha pekee ya njia ya reli kwenye ardhi ya China inayopakana na nchi ya Mongolia, watu wanapenda kuiita sehemu hiyo kuwa ni mlango wa kaskazini wa China. Erlianhaote pia inaitwa kuwa ni "makaburi ya dinosaur" na "maskani ya dinosaur".

    Mji wa Erlianhaote ni moja ya sehemu ambazo visukuku vya dinosaur viligunduliwa mapema zaidi barani Asia. Kutokana na kuweko kwa visukuku vingi vya dinosaur na wanyama wenye uti wa mgongo, wataalamu wa viumbe vya kale waliamua kuuita mji wa Erlianhaote kuwa ni "makaburi ya dinosaur". Kwa sababu mji wa Erlianhaote una aina nyingi za visukuku vya dinosaur, hivyo mji huu ulijenga bustani ya kijiolojia ya dinosaur.

    Bustani ya kijiolojia ya dinosaur ya Erlianhaote imefunguliwa rasmi mwezi Septemba mwaka huu. Bustani hiyo iko kwenye bwawa la chumvi la Errennuoer, umbali wa kilomita 9 kaskazini mashariki mwa mji huu, vitabu vya zamani vya historia viliandika kuhusu sehemu nyingine za mkoa wa Mongolia ya ndani kuhusu kuweko visukuku vingi vya dinosaur. Mara tu baada ya kuingia kwenye bustani hii isiyo ya kawaida, watu wanavutiwa na vielelezo vikubwa vinavyofanana na dinosaur wa kweli wenye uhai pamoja na visukuku vya dinosaur vilivyowekwa kando mbili za njia, vilevile wanashangazwa na milio ya dinosaur, ambayo ilitolewa na vielelezo viwili vya dinosaur vinavyoendeshwa kwa umeme mlangoni mwa ukumbi wa maonesho.

    Hadi sasa ni zaidi ya Yuan milioni 40 zimetumika katika ujenzi wa bustani ya kijiolojia ya dinosaur ya Erlianhaote, ikiwa ni pamoja na ukumbi wa makumbusho wa sayansi ya dinosaur, ukumbi uliojengwa mahali palipofukuliwa visukuku vya dinosaur na ukumbi wa madini yaliyogandishwa. Wakati alipozungumzia kuhusu mpango mzima wa ujenzi wa bustani ya kiikolojia ya dinosaur, mkurugenzi wa idara ya ardhi ya mji wa Erlianhaote Bw Zhang Ruixin alisema,

    "Eneo la majengo ya makumbusho yaliyojengwa kwenye sehemu ya magharibi limefikia mita za mraba elfu 28, fedha zinazotumiwa hadi kukamilisha kabisa ujenzi wake zitafikia Yuan milioni 155, baada ya kukamilika hayo yatakuwa majumba ya makumbusho yanayochukua nafasi ya kwanza duniani kuhusu viumbe vya kale."


    1 2 3
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako