• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bustani ya kijiolojia ya dinosaur ya Erlianhaote

    (GMT+08:00) 2009-10-19 16:59:10

    Kutokana na kufanya ushirikiano kwa juhudi na taasisi ya utafiti wa sayansi za nchi za nje, bustani hiyo ya kijiolojia ya dinosaur imekuwa maarufu duniani. Bw Zhang Ruixin alisema, mbali na watalii waliotoka Asia, kuna vyombo vya habari na watalii wengi kutoka nchi za magharibi wanaofika huko kuangalia. Mwandishi wa habari wa CRI Bi Ashley, ambaye alifika huko kwa kushiriki kikundi cha waandishi wa habari katika harakati inayoitwa "Tazama China --- safari ya waandishi wa habari kwenye sehemu za mpakani", aliona vitu vilivyooneshwa kwenye bustani hiyo vimempa kumbukumbu nyingi, alisema,

    "Nimefurahi sana kufika mahali palipofukuliwa visukuku vya dinosaur. Nilipoona ukanda wa mbuga na eneo kubwa la jangwa, nimeweza kufahamu jinsi dinosaur walivyokimbia kwa kasi wakati ule, na jinsi walivyoishi. Kwetu vilevile kuna majumba ya makumbusho ya dinosaur, lakini mengi ni kama michezo inayotumia sayansi na teknolojia ya kisasa, hayana uzito kabisa, lakini hapa ni penye sifa kubwa halisi, ninaona ni ya kweli kabisa."

    Walioshiriki kwenye kikundi hiki cha waandishi wa habari ni pamoja na Bw Ilija, yeye anaona kuwa bustani ya kiikolojia ya dinosaur inaweka mazingira kwa watu kuwa karibu sana na dinosaur, ili watu waweze kufahamu vizuri zaidi kuhusu kiumbe hicho kikubwa. Anatarajia kuwa watu wengi zaidi duniani wafahamu sehemu hiyo na waweze kufika hapa. Alisema,

    "Hapa kuna watu wengi sana, wanafukua visukuku vya dinosaur kwa juhudi kubwa, na kuwafahamisha watu kuhusu historia ya dinosaur, jambo hilo limenipa kumbukumbu nyingi. Mradi huu unastahili kupongezwa, na unastahili kusifiwa na kuungwa mkono. Ingawa miili ya aina mbalimbali za dinosaur ni mikubwa sana, lakini ninaona wanyama hao ni wema na wapole sana, wanaonekana siyo wa kutisha na wenye hatari sana. Baada ya kurudi nitajitahidi kutoa ripoti kuhusu bustani hiyo, sio tu kutumia maneno, bali pia nitawaonesha watu kuhusu mambo yote ya hapa kwa picha nilizopita."


    1 2 3
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako