Alipogusia ugunduzi mkubwa kwenye sehemu inayojengwa bustani hiyo, Bw Zhang Ruixin alituambia kuhusu ugunduzi wa "jizi dinosaur" wa Erlian. Alisema,
"Hapa ni mahali palipogunduliwa yai la kwanza la dinosaur, liligunduliwa kwenye kando ya ziwa la chumvi. Jina la 'jizi dinosaur' pia lilitokea mahali hapo. Kwa sababu wakati tulipogundua yao hilo la dinosaur, tuliona mifupa ya dinosaur mmoja iko ndani ya yai hilo, mwanzoni tulidhani dinosaur aliiba yai la kasa wa baharini, lakini baada ya wataalamu kufanya utafiti kuhusu ile mifupa ya dinosaur, tukafahamu kuwa lilikuwa ni yai la dinosaur. Tukafahamu kuwa dinosaur walianguliwa katika mayai, wala siyo wanyama wanaozaa."
Ugunduzi kuhusu "jizi dinosaur" unachukuliwa na jarida la The Times la Marekani mwaka 2007 kuwa ni moja kati ya magunduzi 10 makubwa duniani, kisukuku chake kinachukuliwa kuwa ni kimoja kati ya visukuku 8 maarufu vya duniani kwenye mkutano wa wataalamu wa viumbe vya kale uliofanyika mwaka huu.
Bustani ya kiikolojia ya dinosaur ya Erlianhaote inatarajia kufanya uenezi wa sayansi kwa watu wa kawaida hususan kwa watoto, na njia inayotumika ni 'uenezi wa sayansi wa kushuhudia'. Katika siku za baadaye watalii wataweza kushuhudia kazi za ufukuaji wa mabaki ya kale, ambapo watu wenye shauku kuhusu dinosaur watavutiwa zaidi. Bw Zhang Ruixin alisema,
"Tumesanifu vyumba vitano vya wataalamu, ambapo wataalamu na wanafunzi wao watafanya utafiti wa kisayansi, huku watalii wanaweza kuwaona. Mbali na hayo, tumesanifu vyumba vya utafiti kwa ajili ya jumba la makumbusho ya historia ya kimaumbile la Marekani, jumba la makumbusho la Fukui la Japan na taasisi ya sayansi ya Mongolia."
Njia inayotumiwa na bustani ya kijiolojia ya dinosaur ya kuunganisha sayansi ya kiwango cha juu na uenezi wa sayansi, utalii na uzoefu inapendwa na watalii wengi. Bw Li Zongchen ni mwanafunzi wa kidato cha tatu cha chuo kikuu kutoka mkoa wa Shanxi, alipohojiwa na mwandishi wetu wa habari, alikuwa akiangalia wafanyakazi wakichimba ndani ya ukumbi wa makumbusho, alisema,
"Ninaona jambo hili ni muhimu, kwani kwangu mimi ni mara ya kwanza kuona kisukuku cha kweli cha dinosaur, kwa sababu kisukuku cha dinosaur ni kitu chenye thamani kubwa, hivyo sehemu nyingi hazitaki kukionesha kwa watu, bali ni kuwaonesha watu kwa vielelezo. Kwa hiyo ninafurahi sana kupata nafasi ya kufika hapa, kwani nimeona kisukuku cha kweli cha dinosaur."
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |