• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kituo cha mfano cha teknolojia za kilimo ya China chafanya sherehe ya kuweka jiwe la msingi nchini Zimbabwe

    (GMT+08:00) 2009-10-30 15:37:17

    Zimbabwe ina ardhi yenye rutuba, lakini katika miaka ya hivi karibuni, nchi hiyo imekumbwa na msukosuko mkubwa wa chakula, na China ina uzoefu mkubwa katika uzalishaji na usimamizi wa kilimo na teknolojia za kilimo. China inatumia nguvu yake bora ya kilimo kuimarisha utoaji wa misaada ya kilimo kwa Zimbabwe, ambayo itatoa mchango mkubwa katika kutatua suala la chakula kwa wakazi wa huko. Hivi karibuni, kituo cha mfano cha teknolojia za kilimo ya China kilifanya sherehe ya kuweka jiwe la msingi nchini Zimbabwe.

    Kwenye sherehe ya uzinduzi wa ujenzi wa kituo hicho iliyofanyika tarehe 22, wanafunzi wa chuo cha kilimo cha Gwebi kilichoko kilomita 40 ya kaskazini mwa Harare waliandika maneno mapya kwenye wimbo wa jadi wa kabila la Washaona la huko, ili kusifu urafiki wa jadi uliopo kati ya China na Zimbabwe. Mkurugenzi wa kituo hicho Bw. Du Yongqi alifahamisha kuwa, nguvu bora ya China katika mambo ya kilimo itaisadia Zimbabwe kwa kiasi kikubwa kuongeza uzalishaji wa mazao ya kilimo. Alisema,

    "China ina njia pekee ya kuendesha mambo ya kilimo, ingawa eneo la mashamba nchini China ni dogo, lakini kwa kutegemea uzalishaji mkubwa na sifa bora ya kilimo, China inawalisha watu wanaochukua karibu asilimia 25 ya watu wote duniani. Mbinu bora ya China ni kulima kwa makini, na usimamizi wa kisayansi. Naona kuwa labda Zimbabwe ina tatizo la usimamizi mzuri, na matumizi ya mitambo ya kilimo pia si mazuri, kwa hiyo nataka kuijulisha Zimbabwe mbinu bora ya kisasa ya China, ili kuwasaidia kuinua uzalishaji wa mazao wa kila hekta, na kuongeza uzalishaji wa ujumla wa chakula."


    1 2 3
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako