• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kituo cha mfano cha teknolojia za kilimo ya China chafanya sherehe ya kuweka jiwe la msingi nchini Zimbabwe

    (GMT+08:00) 2009-10-30 15:37:17

    Zimbabwe ina mazingira mazuri ya kimaumbile, pia ina miundo mbinu mizuri ya kilimo, na imewahi kusifiwa kuwa ni "kikapu cha mikate" barani Afrika. Lakini kuanzia mwaka 2000 ambapo mageuzi ya ardhi ya Zimbabwe yalipoingia kwenye "njia ya haraka", kwa kuwa wakulima wengi waliopata mashamba mapya hawakuwa na fedha na teknolojia za kilimo zinazohitajika, pamoja na vikwazo vilivyowekwa na nchi za magharibi, uzalishaji wa chakula wa nchi hiyo ulipungua kwa kiasa kikubwa, mwaka 2008 kati ya watu zaidi ya milioni 13 nchini Zimbabwe, milioni 7 walihitaji msaada ya chakula. Waziri wa seriakli za mitaa na miradi ya umma na maendeleo ya miji wa Zimbabwe Bw. Ignatius Chombo alisema, kwa mtazamo wa muda mrefu, ujenzi wa kituo hicho una umuhimu mkubwa katika kupunguza msukosuko wa chakula wa nchi hiyo. Alisema,

    "Kituo hicho cha mfano kitawafanya wataalam wa kilimo wa Zimbabwe wajifunze teknolojia za China za kuzalisha kwa wingi mazao; na watagundua na kupanda mazao yenye uzalishaji mkubwa yanayofaa kulimwa huko; wakulima wanaotoka mikoa na sehemu mbalimbali watanufaika baada ya kutazama wao wenyewe majaribio ya sayansi ya kilimo katika kituo hicho, kadiri muda unavyoenda, ndivyo teknolojia hizo zitakavyoenezwa katika sehemu mbalimbali nchini Zimbabwe; wanafunzi zaidi ya 3,000 wa vyuo vikuu wataona teknolojia hizo za kisasa katika kituo hicho. Kwa ujumla, baada ya wakulima na wataalam wa kilimo kujifunza teknolojia za kisasa za kilimo katika kituo hicho, wataweza kuinua kiwango cha uzalishaji wa kilimo kwa kiasi kikubwa."


    1 2 3
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako