• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kituo cha mfano cha teknolojia za kilimo ya China chafanya sherehe ya kuweka jiwe la msingi nchini Zimbabwe

    (GMT+08:00) 2009-10-30 15:37:17

    Kwenye mkutano wa wakuu wa Beijing wa Baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika uliofanyika mwaka 2006, rais Hu Jintao wa China alitangaza hatua nane za kutoa misaada kwa Afrika, miongoni mwa hatua hizo ni kuimarisha ushirikiano katika mambo ya kilimo, kutuma wataalam 100 wa teknolojia za kilimo wa ngazi ya juu kwa Afrika, na kujenga vituo 14 vyenye umaalum vya mfano wa teknolojia za kilimo. Naibu mkuu wa idara ya uchumi wa vijiji ya kamati ya maendeleo na mageuzi ya China Bibi Fang Yan alisema, kulingana na njia ya zamani ya China kutoa misaada kwa nchi za Afrika bila malipo, sasa kujenga vituo vya mfano vya teknolojia za kilimo kunaweza kuhimiza kwa ufanisi zaidi kuinua kiwango cha ujumla cha kilimo kwa nchi za Afrika. Alisema,

    "Mwaka 2006 baada ya mkutano wa wakuu wa Beijing wa Baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika, wizara za biashara na kilimo zilipanga kwa pamoja mradi huo. Sasa vituo 14 vya mfano vimethibitishwa kimsingi. Kwa kuwa nchi za Afrika zina hali maalum, hivyo China inapaswa kuzisaidia, lakini kama itaendelea kutoa misaada ya bure daima, misaada hiyo itakuwa na kazi ya "kuongeza damu" tu, na sio kazi ya "kuzalisha damu". China inataka kuinua sifa ya nguvu kazi za huko kwa kupitia utoaji misaada ya teknolojia, na kuboresha mitambo ya kilimo, kwa kufanya hivyo, kiwango cha ujumla cha kilimo cha nchi za Afrika kitainuka. Tunayofanya ni kama kupanda mbegu, halafu mbegu hiyo itachipua na kuzalisha matunda."

    Bw. Du Yongqi alifahamisha kuwa, kwa kujaribu kupanda na kuboresha mazao ya kilimo, baada ya miaka miwili au mitatu, mafanikio ya kituo cha mfano yataonekana. Wakati ule, mbegu zinazopandwa kwa kutumia teknolojia za kilimo za China hakika zitazalisha matunda mengi katika ardhi yenye rutuba ya Zimbabwe. Mkuu wa chuo cha kilimo cha Gwebi, ambacho ni mwenzi wa ushirikiano wa Zimbabwe wa kituo hicho Bw. W. matizha alisema,

    "Tuna matumaini makubwa na teknolojia za kilimo za China na moyo wa watu wa China wa kuchapa kazi kwa bidii. Tunakitakia kituo hicho cha Gwebi kiwe kituo chenye mafanikio zaidi barani Afrika."


    1 2 3
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako