• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kijiji cha kale cha Meipi chenye hali ya kuishi kwa mapatano kati ya binadamu na mazingira ya asili

    (GMT+08:00) 2009-11-09 16:29:13

    Mkoa wa Jiangxi uko kwenye sehemu ya kati ya China, toka zamani za kale mkoa huo una utamaduni mkubwa na kutoa mazao mengi ya kilimo. Kwenye kando ya mto Fushui, mji wa Jian, mkoani Jiangxi kuna kijiji kimoja cha kale chenye mambo mengi yasiyofahamika, ambacho kinawavutia watu kutokana na historia yake, majengo mengi ya enzi za Ming na Qing pamoja na sanaa ya uchongaji ya kiwango cha juu. Hiki ni kijiji cha kale cha Meipi, ambacho kinasifiwa kuwa ni "kijiji cha kwanza cha utamaduni wa Luling.

    Kijiji cha kale cha Meipi kiko kwenye umbali wa kilomita 30, sehemu ya kusini mashariki ya mji wa Jian, kwenye tarafa ya Wenpi, sehemu ya Qingyuan ya mji wa Jian, eneo la kijiji ni kiasi cha kilomita moja ya mraba, hivi sasa kijiji hicho kina nyumba 567 na wakazi zaidi ya 2,400. Naibu mkuu wa serikali ya sehemu ya Qingyuan ya mji wa Jianan, mkoani Jiangxi Bw Long Xin, alisema,

    "Kuwa na majengo mengi ya enzi za Ming na Qing ni umaalumu wa kijiji cha kale cha Meipi, ikiwa ni pamoja na utamaduni wa chuo cha fasihi, jengo la kufanyia tambiko kwa mababu jadi wa ukoo, dini, pamoja na sanaa ya uchongaji ya enzi za Ming na Qing. Kijijini kuna mabaki mengi ya kale ya utamaduni ikiwa ni pamoja na majengo 367 ya enzi za Ming na Qing, ambayo yamehifadhiwa vizuri hadi hivi sasa. Kijiji cha kale cha Meipi kimeorodheshwa kuwa kijiji maarufu cha historia na utamaduni cha China na sehemu yenye vivutio ya utalii ya ngazi ya A4 ya nchini China."


    1 2 3
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako