• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kijiji cha kale cha Meipi chenye hali ya kuishi kwa mapatano kati ya binadamu na mazingira ya asili

    (GMT+08:00) 2009-11-09 16:29:13

    Habari zinasema kijiji cha kale cha Meipi kilijengwa kuanzia mwanzoni mwa enzi ya Song ya kusini miaka zaidi ya 800 iliyopita, wanakijiji wote wa kijiji hicho wana jina la ukoo la Liang. Kijijini humo kuna mto mdogo wa Meishui, na neno la Pi la Kichina lina maana ya kando ya mto, ardhi iliyoko kwenye kando ya mto Meishui ni Meipi, hivyo kijiji hiki cha kale kinaitwa kijiji cha Meipi. Kijiji hiki kilijengwa kwa utaratibu mzuri, njia zote zilitandikwa mango pamoja na mfumo kamili wa kuondoa maji ya mvua na maji taka. Kitu kingine kisicho cha kawaida ni mabwawa 28 yanayoungana, tena maji yake yanatiririka. Meneja mkuu wa kampuni ya utalii ya Meipi Bi Yang Caixia alituelezea kazi za mabwawa hayo, akisema.

    "Kijiji chetu ni kijiji cha ikolojia. Mwanzoni mwa enzi ya Song ya kusini kilikuwa ni kijiji kilichojengwa katika mazingira bora yenye milima na mito. Wanakijiji walitegemea mito na maji hayo, ambapo yalianzishwa mazingira mazuri kwa jili ya viumbe na mazingira. Maji yanatoka katika mabwawa 28 yanayoungana, mabwawa hayo 28 yanaitikiana na nyota 28 za mbinguni, hatimaye kijiji hicho kimekuwa katika mazingira hayo. Mabwawa hayo yanaboresha mazingira na kufanikisha shughuli za biashara."

    Shughuli muhimu za biashara za kijiji hicho ziko kwenye mtaa wa kale wa Pitou. Barabara ya mtaa huu ilitandikwa mango, na sehemu yake ya kati ilitandikwa vipande vya mawe ya rangi ya kijivu kali, mtu akisimama kwenye upande wa mwanzo wa mtaa huu wa kale anashindwa kuona upande mwingine. Ustawi wa kijiji cha kale cha Meipi unatokana na mto Fushui. Kutokana na kuweko kwa usafiri rahisi wa majini, shughuli za biashara ziliendelezwa kwa haraka na hatimaye ukatokea mtaa wa Pitou wenye maduka mengi. Meneja mkuu wa kampuni ya utalii ya Meipi Bi Yang Caixia alisema,

    "Mtaa huu wa kale una urefu wa mita 900 na maduka 108. Mtaa huu ulistawi sana hapo zamani. Chini ya vipande hivyo vya mawe ya rangi ya kijivu kali kuna mtaro wa kuondoa maji taka. Kwanza inaweza kuondoa maji taka kwa urahisi; Pili, sisi wachina tunachukulia maji kama alama ya mali, kama maji yanaingia nyumbani, tunaona kama ni ishara ya kukusanya mali. Endapo kuna maji yanayopita milangoni kwa watu, tunaona ni kama mali nyingi zinaingia nyumbani, hiki ni kitu chenye umaalumu kabisa. Tatu, umbo lake ni mfano wa herufi S, sisi wachina tunachukulia umbo la mbuyu kama ni mambo yanayoendelea vizuri, mtaro unavyopita kijijini ni kama umbo la herufi S na ni kama mbuyu, hivyo watu wanaona heri na baraka zinabaki hapa kijijini, kwa kiasi kikubwa hii ni aina ya utamaduni wa maisha, kwani maji yamehimiza uchukuzi wa majini na shughuli za biashara, nyumba zote za kijiji zilijengwa kwa kando ya mtaro huu wenye umbo la S."


    1 2 3
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako