Ili kuhifadhi vizuri kijiji cha kale cha Meipi, serikali ya huko na kampuni ya utalii ya Meipi zimefanya kazi nyingi, zikitarajia kuwa siyo tu limbikizo la kijiji cha kale lililopatikana katika miaka 1000 iliyopita litahifadhiwa, bali vilevile kuhifadhiwa kwa juhudi kubwa kwa mazingira ya maisha yanayoendana na kijiji cha kale. Katika mchakato wa uhifadhi huu, wazo lao moja ni kukubaliana na vitu vya enzi ya kisasa, na kukubaliana na maisha mapya ya mazingira mapya ya kuinuka kwa kiwango cha maisha halisi ya watu. Bi Yang Caixia akisema.
Kwa mfano, kiyoyozi kinaweza kutumiwa, lakini nje ya kiyoyozi tunaiongezea fremu ya mbao ambavyo ni kama kuivisha nguo na kofia. Majengo ya kijiji kizima yana vitu kadhaa hivyo: matofali ya rangi ya kijivu kali, mango, vipande vya mawe ya rangi ya kijivu kali na mbao. Kubakiza vitu hivyo na kuvipamba kwa mbao ili kuepusha kuharibika kwa sura yake kijiji cha kale."
Kadiri jina la kijiji cha kale cha Meipi linavyofahamika katika miaka ya karibuni, hadi sasa kijiji hiki kimetembelewa na watu zaidi ya laki moja, na pato la utalii pia linaongezeka. Kuhusu suala hilo, mwanakijiji wa kijiji cha kale, na mmiliki wa hoteli Yelai ya mtaa wa kale Bibi Liang Libin alisema,
"Shughuli za utalii hapa kwetu zineendelezwa sana, miaka michache iliyopita nilirejea hapa kufungua hoteli, kabla ya hapo nilifanya kibarua katika sehemu za nje. Ni dhahiri kuwa baada ya kufungua hoteli pato langu limekuwa kubwa kuliko zamani. Wageni wengi kutoka nchi za nje wanatembelea hapa. Kuna watu waliotoka Ujerumani, India, na wengine ni wanafunzi wa nchi za nje wanaosoma katika chuo kikuu cha Jinggangshan, vilevile kuna wageni kutoka nchi za nje wanaofahamu na kutaka kufahamu mengi zaidi kuhusu utamaduni wa hapa."
Maendeleo ya shughuli za utalii licha ya kutoharibu mazingira ya kijiji cha kale, pia yamefanya hali ya mazingira ya kijiji cha kale iwe nzuri kadiri siku zinavyopita. Wakati wanakijiji wanapojiendeleza, uelewa wao kuhusu hifadhi ya mazingira unazidi kuimarika. Bi Liang alisema, hivi sasa ni vigumu kuona takataka zinazotupwa chini, watu wote wanaona barabara safi, wanatupa takataka katika mapipa ya takataka. Watoto wanafanya hivyo, sembuse sisi watu wazima."
Kwenye mtaa huo wa kale kwa bahati tuliona kikundi cha watalii waliotoka mkoa Shandong. Watalii walisikiliza kwa makini maelezo ya mfanyakazi wa sehemu ile, na kujionea vivutio vya mtaa wa kale. Mtalii Bi Wang alisema, "Ninapenda sana kijiji hicho, ni safi sana. Hapa kuna vitu vingi vya kale, ni kama tumeletwa kwenye enzi ya zamani. Kijiji cha kale ni kuma kitabu kikubwa, wakati unapofungua ukurasa mmoja baada ya mwingine, bila shaka utavutiwa sana na mambo murua yaliyomo ndani yake."
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |