• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • "Urithi wa Utamaduni Usioonekana wa China"-Usanii wa Nanqu wa Kabila la Watujia, China

    (GMT+08:00) 2009-11-09 16:19:53

     

      Nanqu ni usanii wa muziki unaochanganya kuimba na kuongea katika wilaya inayojiendesha ya Changyang ya kabila la Watujia, kusini magharibi mwa mkoa wa Hubei China. Usanii wa Nanqu unavutia kutokana na sauti yake inayoeleza hisia.

      Hapo kale wilaya ya Changyang wanayoishi Watujia ilikuwa ni makutano ya utamaduni wa dola la Ba na utamaduni wa dola la Chu, kwa hiyo sanaa ya wilaya hiyo ina mchanganyiko wa tamaduni za madola hayo mawili. Mkuu wa ofisi ya kuhifadhi utamaduni wa jadi wilayani humo Bw. Dai Zengqun alisema, sanaa ya Nanqu ni matokeo ya mchanganyiko wa utamaduni wa kabila la Wahan na kabila la Watujia. Alisema,

      "Nanqu ni usanii wa muziki wa jadi katika mkoa wa Hubei, Usanii wa Nanqu inarithishwa miongoni mwa wasanii kizazi kwa kizazi, kwa mujibu wa ala zake za muziki, Usanii wa Nanqu iliibuka wilayani humo zaidi ya miaka mia mbili iliyopita."

      Kwa sababu hakuna wasanii wa kulipwa wanaoshughulika na Usanii wa Nanqu, kuhifadhiwa kwa Usanii wa Nanqu kunategemea washabiki kufundishana kizazi kwa kizazi. Hadi leo wenyeji wanaposherehekea harusi, siku za kuzaliwa au sikukuu fulani huwa wanakusanyika pamoja wakiimba huku wakipiga kinanda. Katika kijiji cha Ziqiu, karibu kila siku giza inapotanda sauti za vinanda kutoka majumbani husikika.


    1 2 3
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako